Thursday, February 21, 2019

KUZALIWA MARA YA PILI


Tunaishi katika hii dunia kwa jinsi ya mwilini na rohoni  pia tunatumia akili na nguvu ili kufanikisha shughuli zetu. Kuna wakati tunatumia nguvu sana kuliko akili, na kuna wakati pia tumia akili sana kuliko anguvu hata wakati mwingine vyote vinatumika pamoja.

Tunapo ongelea akili tunaongelea ufahamu na maarifa ya mambo flani, pia kuhusu mwili, roho na nafsi; navyo vinatakiwa vifanikiwe kwa namna flani. Mtume Yohana atatutakia heri akisema  mpenzi naomba ufanikiwe kama nafsi yako ifanikiwavyo. Mungu anatamani tufanikiwe ki mwili ,roho, nafsi,na akili. 

Je tutawezaje kufanikiwa?




YOHANA 3 : 3 Yesu akajibu akamwambia amin, amin, nakuambia,  mtu asipozaliwa mara ya pili, awezi kuuona ufalme wa Mungu.

Katika kitabu cha yohana tunakutana na hii stori ya mfarisayo aitwaye Nikodemo ambaye alikuwa mkuu wa dini ya wayahudi na pia ukiendelea mbele Yesu anatutambulishia kuwa huyu mtu alikuwa ni mwalimu wa Israel. Kwaiyo alikuwa anaufahamu na maarifa kuhusu mambo flani flani. Hatukuambiwa alikuja kwa madhumuni gani kumuona Yesu lakini tunaona kuwa Yesu alimjibu kuhusu kuzaliwa mara ya pili. Kwa maana alijua ya moyoni mwake kabla hajauliza
 Tunaweza tukasema kuzaliwa kwa mara ya pili  ni kumkiri Yesu kuwa Bwana na Mokozi wa maisha yako na kulifata jinsi Neno lake linavyosema na kuishi jinsi alivyotaka tuishi na kubatizwa kwa maji na Roho mtakatifu yaani kuuzika utu wa kale na kufufuka na utu mpya.,


FAIDA YA KUZALIWA MARA YA PILI.

1.    Kusamehewa dhambi

Ukizaliwa mara ya  pili unakuwa ndani ya kristo na unakuwa kiumbe kipya na Mungu wa mbinguni anasamehe dhambi zako na kukuweka ndani ya pendo lake ambalo ndani yake kuna Baraka na neema, 

ukisoma  2WAKORITHO 5:17 inasema Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya kristo,amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita; Tazama! Yamekuwa mapya

2.    Kuhesabiwa Haki

1YOHANA 2:29 inasema kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendae haki amezaliwa na yeye

Tunajua kuwa  tunahesabiwa haki kwa imani; kama haujazaliwa mara ya pili huwezi kuhesabiwa haki kwa kuwa sheria inakufunga. Lakini ashukuriwe Mungu baba aliye mtoa mwana wa pendo lake takatifu {YESU} kufa pale msalabani kwa ajili ya dhambi zetu ili zambi zetu zoote ziingie kwake ndani ya mwili wake na baada ya mateso yote na akasema IMEKWISHA. Kwaiyo ndugu kama Yesu alimaliza yote pale msalabani sisi tuliozaliwa mara ya pili tunahesabiwa haki kwa imani. 

3.     Hutokufa bali utaishi

tunasoma katika MATHAYO 27: 51 -53  anasema Na tazama pazia la hekalu likapasuka  vpande viwili toka juu hata chini ; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifuwalio lala; 53nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.

Tunaweza kujiuliza kivipi? YESU alivyo fufuka, akufufuka peke yake alifufuka na wafu waliokufaga zamani wale walio wake yaani watakatifu. Kwaiyo tukifa katika mwili huu tunakwenda directly mbinguni tukisubili ile siku kuu ya mwana wa adamu kuja ulimwenguni kwa mara ya pili. 1YOHANA 4: 9b inasema ili tupate uzima kwa yeye

Faida ziko nyingi sana na sana  ambazo utazipata kwa kulisoma neno lake.
 Rafiki
Kama ujampokea Yesu kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako nakuomba useme kwa sauti na kwa kwa kumaanisha na kuamini moyoni mwako maneno haya.


BWANA YESU NAKUJA MBELE ZAKO, MIMI NILIE NA DHAMBI

SIKUSTAHILI KUISHI SIKU YA LEO, LAKINI NI NEEMA YAKO NA REHEMA,

NATUBU ZAMBI ZANGU, NILIZOZIFANYA KWA KUNENA KWA KUTENDA NA KUWAZA

NAOMBA UNISAMEHE MIMI NILIE NA DHAMBI, NAKIRI KUWA WEWE NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU,  FUTA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, ANDIKA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA UZIMA.  ASANTE YESU KWA KUWA UMENIOKOA. AMEN

 Kama umesema hayo maneno, hakika Mungu amekusamehe kabisa na amesahau dhambi zote ulizofanya , unatakiwa uende kanisa lililo kalibu nawe ili upate mafundisho na kukua kiroho.
                                          MUNGU AKUBARIKI……
.

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...