Mathayo 8:1-4
Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.
Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika.
Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
Shalom natamani tukumbushane habari hii ya mtu mwenye ukoma .... ambaye Yesu kristo wa Nazareti alitamani amponye huyu mtu kwakuwa alifanya vitu vifuatavyo÷
1. Alipokuja huyu mtu alimsujudia kwa kuonesha Heshima yakuwa Yesu ni Mfalme wa Ulimwengu
2. Alikuwa na imani yakuwa Yesu ni mkombozi wa ulimwengu na atamponya
Katika mstari wa nne Yesu anasema ukaitoe sadaka na iwe ushuhuda kwao.
Why tunatoa sadaka ?
Kwa sababu tunashukuru kwa Yale Mungu aliyotutendea.... kwa maana nyingine tunatambua ukuu wake kwetu.
Kunakitu kakiongelea cha ushuhuda... ushuhuda una nguvu sana. Unaposimama kutoa ushuhuda unamaanisha vitu vifuatavyo÷
1. Unamtukuza Mungu
2. Unamuaibisha shetani (ufunuo 12÷11)
3. Unawafundisha watu kwa Mungu hata ili linawezekana
4. Unakuza imani za watu zilizo haba
Zaburi 71÷15-18
Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako Mchana kutwa; maana sijui hesabu yake.Nitakuja na mambo ya ajabu ya Bwana MUNGU; Nitawakumbusha watu haki yako Wewe peke yako.
Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.
Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
Napenda sana mstaribwa 16... nitawakumbusha watu haki yako ... Mungu anatutendea makuu ili sisi watu wake tuwe walimu... mana kuna watu hawaamini bila mifano ...
Zaburi 119÷46
Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu.
Mwimba zaburi anamwambia Bwana kwamba atazinena shuhuda za Bwana mbele ya watu wakubwa wa dunia wala hataona aibu... anatufundisha kuwa Mungu yeye ndiye aliweka hao wafalme huna haja ya kuona aibu ...kuna watu wanaogopa kutoa ushuhuda kwa sababu ya kuonekana na jamii iliyo mzunguka..... anasahau kuwa ushuhuda una nguvu... ushuhuda unamuabisha shetani....
HALELUYAH!

Its really encouraging word of God, it makes my heart flow with great joy from the Most High
ReplyDelete