amen
SEMINA YA NENO LA MUNGU ILIYOFUNDISHWA NA MWALIMU CHRISTOPHER
MWAKASEGE JIJINI DAR ES LAAM.
SOMO: MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO
▶Lengo
Kuweka ndani yako maarifa ya
Kibiblia yatakayokuwezesha kutumia fikra zako ili ufanikiwe ktk maisha yako
Mith 23:7(a)
Tafsiri zingine neno aonavyo
nafsini mwake:-
1. afikirivyo nafsini mwake
2. awazavyo nafsini make
3. anavyotafakari nafsini
mwake
Mara nyingi kwenye Biblia
utakuta fikra imeandikwa fikira ni neno lilelile
MAANA YA FIKRA
Ni mkusanyiko na mtiririko wa
mawazo unaotengeneza maimamo wa kiutekelezaji ndani ya mtu.
UNAJIFUNZA NINI AU UNAPATA NINI KUTOKA KWENYE TAFSIRI
HIYO YA FIKRA
⃣
Ulivyo kimaisha iwe kiroho au kimwili ni matokeo ya jinsi uonavyo/ufikirivyo
nafsini mwako.
2⃣Ulivyo kimaisha inaonyesha kiwango chako cha kufikiri
kilipo au kilipofikia
3⃣Fikra ziliumbwa zikae ndani ya nafsi ili zitumike
kuweka aina na kiwango cha maisha ya mtu ktk eneo linalomuhusu!
Kumbuka mtu ni roho anayo
nafsi anakaa ktk mwili. Nafsi ni kiungo cha kati kati ya roho na mwili kuweza
kusaidia kutafsiri roho kuishi ktk ulimwengu wa mwili bila shida na mwili
kuishi ktk ulimwengu wa roho vivyo hivyo.
✳Ndani
ya nafsi kuna fikra na akili pia
✳Ndani
ya mwili kuna ubongo
Kwa hyo kiwango cha
kufanikiwa kimewekwa kwenye nafsi=fikra
4⃣Tofauti ya aina ya viwango Vya maisha kati ya mtu na
mtu inatokana na sehemu kubwa na utofauti wao wa kufikiri
2Kor 11:3
➡Shetani
akitaka kukumaliza aanzi kwenye roho bali uenda moja kwa moja kwenye
nafsi=uvuruga fikra zako kwanza
➡Kwenye
Bustani ya Eden
alivuruga fikra zao kwanza vivyo hivyo kwenye swala la mtu kuokoka kule
kusitasita na kuamua vinginevyo ni fikra uvurugwa kwanza.
HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA
FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA
1⃣Tasmini maisha yako I'll ujue kiwango cha kufikiri
kwako kilivyo
✅Haijalishi mahali ulipo au maisha uliyonayo mazuri ama
la
✅Itakusaidia ujue unaanzia wapi ktk kushughulika na
kufikiri kwako
✅Kama unataka kwenda na BWANA kwenye jambo lolote
jifunze kuanza na kuwa unajitathimini kila wakati!
✅Wengi ujiuliza natumia vigezo gani kujitathimini?
Kiblia kigezo cha maisha ni
Agano
Ndani ya Agano YESU KRISTO
aliweka viwango Vya maisha ambavyo vitatusaidia ktk tathimini
MIFANO YA KUJIFUNZA HAPA
2Falm 4:1-7
Maisha ya mama mjane
tuyatafakari ili tuweze kujua kiwango cha kufikiri kwake
TUNAONA MAMBO YAFUATAYO
1. Fikra zake za kimaisha
zilikwamia mahali zilipokwamia fikra za mume wake.
✅Maana yake hakuwa na mawazo ya kimaisha zaidi ya yale
ya mume wake mpaka pale mime wake alipofariki.
KIVIPI
-Sababu fikra hazipo hakuwa
na hakujua kitu cha kufanya ndo maana alimwendea Elisha.
✅Ile kwamba umeolewa haifanyi kwamba akili yako
isifanye kazi au ya mime wako ndiyo sahihi na superior tu.
2. Hali ya maisha na kiwango
cha maisha cha mama mjane na watoto wake kilitokana na ulipofika mtiririko na
mkusanyiko wa fikra za mume wake.
✅Ukitaka kujua yule baba alifikirije angalia maisha ya
familia take
✅Kuishi kwako ni matokeo ya kufikiri kwa baba yao .
✅Umaweza ukawa na maisha mazuri kumbe ni fikra ya
kampuni unayofanyia kazi
3. Fikra za mume wake
zilitengeneza viwango Vya maisha yake na familia kutoka kwenye maeneo haya
yafuatayo:-
(a) Kulitegemea Utumishi wake
aliokuwanao kwa Elisha
(b) Kumcha BWANA ilikuwa ni
kigezo cha maisha yao
(c) Alikuwa anaishi kwa mkopo
na ambao alikufa hajaumaliza
✅Kumbuka Utumishi hautengenezi maisha yako Bali FIKRA
✅Biblia haikatazi mkopo bali deni
✅Usifurahia uchaji tu ulionao kama
uchaji huo hauwezi kuchaji fikra zako huwezi kufanikiwa kimaisha japo mbinguni
utaenda.
4. Mume wa mjane alimjengea
mkewe kufikiri ya kuwa maisha yao
yalitokana na ushauri na mwongozo wa Elisha na kumbe siyo
5. Mama mjane hakujua cha
kufanya juu ya fikra za mume wake ya kuwaweka watoto rehani
✅Aliwaweka watoto rehani maana yake alikuwa anawajengea
watoto wake fikra za utumwa
6. Fikra zake na mume wake
hazikuwa na uwezo wa kutumia walichokuwanacho ili kuwatengenezea maisha mazuri.
HOME WORK
Jiulize maswali haya
1⃣Jiulize nini chanzo cha kipato chenye kufanya uwe
jinsi ulivyo?
2⃣Je chanzo hicho kikiondoka/kutoweka je maisha yako
yatakuwaje?
3⃣Fikra zako zinahusika kwa kiwango gani ktk kupatikana
kwa kipato hicho?

No comments:
Post a Comment