Saturday, March 27, 2021

Yesu kiongozi Mwema

Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.
Mt 9:2‭-‬6 SUV

Kiongozi wetu Yesu kristo anatufundisha vitu katika sura hii jinsi alivyo kutana na changamoto au jina lingine niite jinsi ya alivyokutana na  fursa ya kumponya mwenye kupooza

Kuna vitu vinne ambavyo anatufundisha katika mistari hii.

1. Huruma
Tunaona Yesu kristo kama Mungu mwanadamu aliyekuwa na uwezo na mamlaka ya kufanya chochote hapa duniani alikuwa na huruma kwa wanadamu ,  kama alivyo mwambia Yule mwenye kupooza 
Jipe moyo mkuu mwanangu, umesamehewa zambi zako
Tukisoma hayo maneno aliyosema Yesu tunakuta anatufundisha kuwa tunatakiwa tuwe na moyo wa huruma wakusaidia watu kwa njia yoyote.  Awe mwamini au sio mwamini kwa sababu ni moja ya jambo jema kwa Bwana.

2. Mamlaka
Wakristo wwngi sana huwa tunaogopa kutamka vitu vya mungu vilivyo moyoni kwakuwa tunaogopa kama watu watatusema vibaya na kutuona tuna makosa. Lakini tunasahau ya kuwa tumepewa mamlaka  na funguo Juu mbinguni na Duniani,  kwa kila jambo jema lenye kumpendeza Mungu  kwa sababu kwa kila mambo safi Roho mtakatifu hufanya kazi na hao wafanyayo hayo.
Lakini paulo mtume wa Yesu anatukumbusha kuwa tunatenda kazi kwa kadri ya nguvu ifanyayo kazi ndani yetu. Kwaiyo hatutakiwi kuogopa  kufanya jambo jema ambalo mamlaka ya mbinguni inakubaliana na sisi,  Yesu alikuwa na mamlaka ya kumponya na kumsamehe yule aliye pooza kwa kiwa lilikuwa ni jambo jema.

3. Uweza
Watu wengi tuna changamoto ya kubadili tafsiri ya mambo ya rohoni kuwa katika mwilini (physical)  
Yesu alikuwa na uwezo wa kutamka kilicho rohoni kwake kikawa katika hali ya mwilini,  

Je kwanini vitu vya rohoni havitokei kwa jinsi ya mwilini?

a. Hatuombi sawasawa na mapenzi ya Mungu
b. Hatuna mbegu ya imani.

Hizi ni baadhi ya vitu ambavyo vinafanya vitu vya rohoni kuonekana katika ulimwengu halisia . 

4.kutia moyo au kusaidia huduma au kazi za watu wengine.

Yesu kristo kiongozi wa imani yetu 
Aliona imani na juhudi ya wale watu ambao walimbeba ndugu mwenye kupooza.
Hivyo akafanya huduma ya kumponya yule mtu,  na tunaona watu wengi wanashindwa kuona juhudi  za watu wengine  na hata kuwatia moyo , hata pengine  kuwapa neno la hekima ili wasonge mbele katika familia zao, 
Lakini pia hata kuomba pamoja nao, katika hali wanayo pitia,  maana tunaona hata Yesu  aliwachukua baadhi ya wanafunzi kwenda kuomba nao mlimani, na hii inatufundisha kuwa alitaka wamtie moyo katika hali zote za huduma yake,

Lakini hata alipofunga siku 40, tunaona kuwa malaika walikuwa pamoja nae wakimhudumia, 
Lakini pia hata musa na eliya walishuka kumtia moyo...

Mwisho Yesu kabla ajampa uponyaji huyu mtu mwenye kupooza alianza kwa kumwambia habari njema . Umesamehewa dhambi zako.  hivyo basi katika huduma yoyote tunatakiwa tuna waambia watu habari njema za Mungu.



No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...