Tuesday, September 29, 2020

ROHO YA MATENGANO

Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.

1 KOR. 1:10 

Mtume paulo anatukumbusha kuwa  katika maisha ya kila siku tujitahidi sana tuwe tunaongea lugha moja au jina lingine tuongee vitu vyenye maana moja, ili kati yetu kusiwe na mgawanyiko.   

Hii tumeiona baada ya watu walipogaqanyika wengine wa paulo na wengine apollo.

That means apollo alikuwa na aina yake ya kufundisha na paulo pia. Kwaiyo watu wakajikuta wanatafuta ubora . Ambacho hicho kitu hakitakiwi  kabisa katika huduma ya Mungu, 

2. Pia mafarakano mengi yanatokea pale ambapo watu walio elimika wanataka kusikilizwa  na kupuuzia mawazo ya wengine

Nikwambie kitu , biblia inasema kuwa tufanye kazi ya Mungu kwa hekima yote, ana maana kuwa tujitahidi sana kutumia hekima ili Neno la Mungu lipokelewe kwa furaha.

3. Kutumia hekima ya kukaa kimya.

Biblia inatufundisha  ni heri kuwa msikilizaji utaonekana kuwa una hekima kuliko kuwa miongeaji. Lakini pia hii inatukumbusha wakati wa esta na naamani, esta alipo sikia yale mambo alikaa kinya na kufunga kwa siku tatu ili apate kibali kwa Mungu na kwa mfalme, ili aliseme jambo lake. Lakini tunaona kuwa alifanikiwa ,  biblia inasema kuna wakati wa kusema na wakati wa kunyamaza. So ukiona kuna mtafaluku katika kundi au kanisa au familia kaa kimya kwa muda tafuta hekima ya Bwana ,ili usubiri hekima ya kimungu ije juu yako.

4. Kutii 

Biblia inatuhimiza kuwa tutii amri iliyo kuu. Maana zote zinatoka kwa Bwana.  Endapo katika uongozi wa kitaifa, nyumba au kanisa au jamii. Kama kuna wazo hujapendezwa nalo basi kutii ni bora kuliko mafuta ya beberu. Maana Bwana anajua na  anasababu,  tunakumbuka stori ya nebukadreza alivyoambiwa na Bwana kupitia maneno ya mtumishi wake danieli kuwa aweke sawa ufalme wake kabla ya kuharibiwa. Alipuuzia na akaishi misimu mingi kama mnyama. Lakini baadae aliludi kwenye uongozi na kuandika Mungu wa danieli ni Mungu wa kweli. 

Ili tusiweze kufarakana ni bora tuwe tuna tii, maana Bwana anataka tuwe wana maombi , tumuulize yeye kwanini hili linatokea, naye atatupa kujua na1 kurekebisha . 

Ni maombi yangu kwa ajili yako.

Bwana akupe moyo na tunda la uvumilivu, 

Bwana Akupe tunda la kupokea mafundisho ya watumishi mengine

Bwana akupe roho ya hekima 

Bwana akupe roho ya umoja

Bwana aondoe roho ya matengano

Amen...

No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...