Friday, September 23, 2016

YESU ANATHAMINI MUDA WAKO


MHUBIRI 3:1-8                                     ukisoma huo mstari utajifunza kuwa Kuna wakati kwa kila kitu kilichopo duniani..,Mungu aliviumba vitu katika mifumo tofauti ambazo zinaenda kwa  muda na wakati.

Na kuna nyakati na misimu kwa kila shughuli zinzo fanyika duniani
Mfano kipindi cha masika na kiangazi
Binadamu naye ameubwa katika kupita katika vipindi tofauti , ndo mana biblia inasema kila jambo na wakati wake. Kuna wakati mwanadamu anapita katika majonzi ,lakini hayatokuwa ni maisha yake yote, na kunawakati mwanadamu anapita kwenye furaha lakini haitakuwa maisha yake yote.

Kuna majira lazima mwanadamu apite ili yamfundishe na kumfanya awe jasiri akikutana na changamoto kama hile iliyopita

MWANZO 1:14
.Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye
nafasi ya anga ili itenganishe mchana na usiku, nayo iwe  alama  ya kutambulisha majira mbali mbali, siku na miaka,


Nataka tutazame alipo sema ALAMA  …hapa tunaona kuwa Mungu aliweka sign kwa kila majira yanayotaka kutokea , ni sawasawa na kwa  mwanadamu kila changamoto inayotaka kutokea maishani mwako lazima kuwe na alama, iwe umeokoka au ujaokoka, Kwa sisi tulio okoka Roho wa Bwana ndie hutupa ALAMA za majira na nyakati.

                                         
MUWEKE YESU ASHIKILIE MUDA WAKO

kwamba mpango wa Mungu kwa mwanadamu ni Mzuri, mwanadamu alijichanganya na kutofautiana na Mungu pale alipotenda dhambi, na kuna majira yaliwekwa kuwa ATAFANIKIWA KWA  JASHO LAKE MWENYEWE ,

Tunajua kuwa hii hali ilikuwa ni ngumu sana , lakini Mungu wa Israeli akamtuma mwanawe wa pekee yesu kristo aje duniani ktupa ukombozi na ile neema itoka nayo na ukombozi,

Kwa mtu ambaye amemkiri Yesu kuwa ni Bwana na mokozi wa Maisha yake, Yesu anakuwa ni kiongozi au dereva wa majira na nyakati zilizo wekwa maishani mwako. Na kila changamoto itakayo tokea Roho mtakatifu atakujulisha ili ufanye maombi .

Tena yesu awezi kukuacha katika changamoto unazopitia kwa kuwa umemueka yeye awe kiongozi wako wa kila kitu.



ISAYA 60:19-20
19Jua halitakuwa tena nuru yako mchana,
wala mwangaza wa mwezi
hautakuangazia,
kwa maana BWANA atakuwa nuru
yako ya milele,
naye Mungu wako atakuwa utukufu
wako.
20Jua lako halitazama tena,
nao mwezi wako hautafifia tena,
BWANA atakuwa nuru yako milele,
nazo siku zako za huzuni zitakoma.

Hapa tunajifunza vitu vingi sana, kimoja wapo ni Yesu atakuwa utukufu wako, kivipi ? 
pale utakapo muweka awe kiongozi wako kwenye kila kitu, hata kwenye masomo
Nimeona wanafunzi wengi wakiwa bize na time kwenye kusoma but wanamsahau yesu ambaye anauwezo wa kubadilsha mawazo na upeo wa akili zao kwa sekunde chache.

Pia tunaona kuwa watu wengi hutazama jua na mwezi na hata nyota kujua nyakati na majira lakini pale utakapo mweka Yesu mbele, utukufu utaonekana katika majira yote utakayo ishi.

Pia unakuta mwanafunzi anajali muda wa kusoma kuliko kufanya maombi,kuliko kusoma biblia angalau kwa  nusu saa. Ukimweka Yesu awe kiongozi katika muda wako, Hakika atakuwa utukufu wako na hata katika siku zako za shida Yesu ataziondoa kwa kuwa umemuweka yeye awe kiongozi wa muda wako

YOHANA 1:1-4
Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.
3Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 4Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu.

Katika mistali hii tunaona kuwa Yesu kristo alikuwako tangu mwanzo wa kuumba dunia, tena ndani yake kunako uzima na milele na huo uzima ndio nuru ya watu… kwa hiyo kama uzima ni nuru ya watu basi katika uzima anaotoa yesu ndipo tutafanikiwa kuukomboa wakati na majira… kitakacho tusaidia ni kufanya maombi kwa bidii.





No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...