
KUELEKEA 2019
Kuna wakati nakaa kujiuliza tofauti kubwa ya 2017 na 2018 itakuwa ni nini haswa? Siku zitaendelea kuwa vile vile au zitabadilika, au kuna mabadiliko gani haswa yatafanyika ,2017. Serikali itabaki kuwa ile ile na hata sisi tutaendelea kuwa wale wale au kuna kitu cha ziada kitatendeka.... Au ni mabadiliko ya kuama kwenye namba 7 na kuingia 8?
Hayo ni miongoni mwa machache yanayonijia akilini kunifikiriza.
Kabla ya kuingia 2019 na kauli za kujitia moyo tumia muda wako na ujiulize maswali haya....
1. Ktk malengo ya 2018 niliyojiwekea January mangapi yametimia na mangapi hayajatimia?
2. Vipi ni vikwazo vya kutotimiza malengo?
3, yaliyotimia yametimia kwa kiwango gani?
4. Na si vibaya kujihoji umeongeza mtandao wa watu muhimu maishani mwako kwa kiasi gani?
Na maswali mengineyo mengi ya muhimu. Jihoji maswali haya yatakusaidia kukuandaa kufanya vyema zaidi 2019.
Ukitazama list ya malengo ya 2018 utagundua kuna mengine ulikurupuka kuyaandika hukuzingatia uhalisia. Unapoelekea 2017 hakikisha unatulia kupanga mambo ya kufanya kwa utaratibu na si kwa hisia zaidi.
MAMBO YA MSINGI KTK KUPANGA YA KUTEMBEA NAYO 2019
1. Panga mambo ambayo yanatimizika. Usikurupuke kupanga tu bila kujifanyia tathmini binafsi. Weka list ya mambo ambayo utayatekeleza.
2. Usipange kwa kufuata mkumbo.
3. Jiwekee nidhamu ya kutembea ktk muda ktk Yale uliyoyapanga. Uwe na deadline ktk kila unalolipanga kulifanya. Deadline itakuchochea kutotulia.
4. Ongeza maarifa zaidi ya 2018 ili yakusaidie kutekeleza malengo uliyonayo. Soma! Soma!
5. Epuka kabisa vitu vitakavyokukwamisha kufikia malengo yako.
6. Mtegemee Mungu ktk yoteUliyonayo naye atakufanikisha.
Usisahau kuwa kama hautabadilisha namna ya kufanya hakuna tofauti yoyote ya 2018 na 2019.
Ukitaka kuona mabadiliko Fanya zaidi ya 2018.
Heri ya mwaka mpya.(From Brother wanguu Kelvin Kitaso)
No comments:
Post a Comment