
..KUTATHIMINI FIKRA ZAKO
Je? Unajuaje kuwa
unachomuomba Mungu akufanyie ndicho mapenzi yake?
Warumi 8:26-28
Na yeye aichunguzaye mioyo
aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama
apendavyo Mungu.
27 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu
hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa
kwa kusudi lake.
Roho Mtakatifu ni Mungu ndani
yako. Ni muwakilishi wa Mungu ndani yako. Muulize Roho Mtakatifu nini uombe.
Roho Mtakatifu ataweka neno ndani yako. Yeye huomba sawa na mapenzi ya Mungu. Kama una neno ndani yako utajua tu. Kwenye nafsi kuna
nia,hisia nk. Roho Mtakatifu
atakusaidia.
Funzo la kwanza
Usizuie fikra zako
kushughulika na swali ambalo hujui kwanini limeulizwa. Swali la Elisha na jibu
la yule mama yalikuwa tofauti kabisa. Mama hakujua kwanini swali limeulizwa na hilo likamuwekea mama
ukuta ili fikra zake zisifike mbali. Ndio mana wengi wakiwa kwenye hali hii
hupenda zaidi ya kuombewa kuliko kuelewa tatizo. Unapoulizwa maswali na
mtumishi usimkatishe kuuliza. Huwa kuna sababu. Unapoulizwa swali ambalo Mungu
tayari ana majibu nalo tatizo lipo kwenye fikra zako.
Funzo la Pili.
Swali la pili liliulizwa
kwakuwa swali la kwanza halikufaulu kuamsha fikra za mama mjane kufikiri zaidi
ya pale zilipokomea kufikiri. Mama alieleza shida zake lkn sio anataka nini!
Kazi ya swali la kwanza lilikuwa kwa ajili ya kuamsha fikra za yule mama ndio
mana likaulizwa la pili. Fikra zilizochoka kufikiri unazipa mzigo kufikiri kitu
cha pili. Haijalishi unajaza mafuta kiasi gani kwenye gari engine ikiharibika
ni kazi bure. Wazo jipya kwenye fikra zilizochoka ni kazi sana . Inawezekana Mungu anataka kuyapekeka
maisha yako kiwango kingine lkn wewe unaona umechoka.
Fikra za Yesu zilichoka kabla
ya kusulibiwa ndio mana wakaja malaika kumtia moyo. Mwili ukiwa umechoka
akashuka mlimani. Mungu alimtia nguvu Yesu ili amalizie safari yake atakutia
moyo na wewe. Ndio mana misuli ya anayepanda lift na anayepanda ngazi huwa ni
tofauti. Mungu anatafuta kinachopatikana
kwako pale anaposhughulika na wewe
Mithali 3:5
Mtumaini Bwana kwa moyo wako
wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Kuna tofauti ya kutumia akili
zako na kuzitegemea akili zako mwenyewe. Yani usiziache akili zako zikafanya
kazi zenyewe. Akili zako hazikuumbwa zifanye kazi zenyewe. Angalia mwanadamu
anapoumbwa anapuliziwa pumzi ya Mungu. Ukiwa mwanasayansi unaona oxygen lkn
kiroho ni pumzi ya Mungu. Ni zaidi ya pumzi ya kawaida. Akili ziliumbwa zifanye
kazi na Roho Mtakatifu na neno
Luka 24:45
Ndipo akawafunulia akili zao
wapate kuelewa na maandiko.
Yesu alizifungua akili zao
ili wawe mashahidi wake. Wasingeweza kufanya kazi bila Roho Mtakatifu na neno
ambalo lilikuwa kwa ajili ya kuwasaidia.
2 Timotheo 3:16-17
Kila andiko, lenye pumzi ya
Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao , na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha
katika haki;
16 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa
apate kutenda kila tendo jema.
Isaya 55:8-11(isome )
Akili zetu hazikuumbwa
kutumia neno na roho nyingine zaidi ya ile ya Mungu. Ili shetani
aweze kutumia akili zetu aliharibu fikra kwanza. Tushindwe kutambua tubebe tu
hata mabaya. Ndio mana swali la pili lilikuwa muhimu sana ili kuamsha fikra. Ndio mana unapopita
kwenye magumu mengi unakuwa na maswali mengi kuliko majibu. Mengine huwa ya
Roho Mtakatifu. Ndio mana hata kama anajua
unachotaka bado alikupa akili zitumike. Usitumie akili bila roho wa Mungu. Ndio
mana tunakwama maishani. Kuna waliookoka wamekwama na wasiookoka wanafanikiwa
mbele.
Funzo la Tatu.
Angalia/Orodhesha vitu
ulivyonavyo hata kama unaona havina thamani.
Yule mama alipoulizwa ana
nini cha kwanza alisema hana kitu. Hakujua kwanini swali linaulizwa. Kwa lugha
nyingine alikuwa anamwambia Elisha nilivyonavyo havina thamani ya kunitoa
nilipo.
Mithali 14:13-21
Yesu akatoka, akaona mkutano
mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.15
Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa
ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini,
wakajinunulie vyakula.
16 Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao,
wapeni ninyi vyakula.
17 Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate
mitano na samaki wawili.
18 Akasema, Nileteeni hapa.
19 Akawaagiza makutano waketi katika majani;
akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni,
akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa
makutano.20 Wakala wote wakashiba;
wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili,
vimejaa.21 Nao waliokula walikuwa
wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.
Yesu anawauliza wanafunzi
wake. Kwanini mnataka watu hawa waondoke? Yesu anataka kushughulisha fikra zao.
Alipowaambia kuwa wawape chakula akili yao
ikaweka defence kuwa hakuna Chakula. Lkn Yesu anaona kuwa wanafunzi hawana Neno
wanaangalia nje na sio ndani. Mungu ametuumba kwa namna ambayo msaada utaanzia
ndani. Hata wewe orodhesha una vitu vingapi hata kama
vya kurithi? Usiseme huna kitu. Hata kama ni pikipiki mbovu. Ndivyo hata kwenye
kampuni yoyote wanavyofanya INVENTORY. Unahesabu vyote. Kisha angalia vipawa
ulivyonavyo. Mfano unachekesha wenzio kijiweni bure lkn wenzako wanatumia huo
uchekeshaji wanapata hela. Andika vyote! Usiangalie thamani
Funzo la nne
Unahitaji kujua kwa msaada wa
Mungu kwanini unacho ulichonacho? Kwanini? Kwasababu thamani yake inategemea
uhitaji wake. Yule mama alijua ana chupa ya mafuta lkn hakujua kwanini anayo.
Kwahiyo hakutumia alichokuwa nacho ipasavyo?
2 Wakorintho 9:10
Na yeye ampaye mbegu mwenye
kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye
atayaongeza mazao ya haki yenu;
Je,ulichonacho ni mbegu au
mkate. Anayeamua ulichonacho kiwe mkate au mbegu ni Mungu. Anakupa mbegu na
mkate. Nani anayeamua mbegu iwe mbegu au mkate kama
mkate sio Mungu bali Fikra zako. Haijalishi amekupa mbegu au mkate anategemea
ushirikiano wako. Ukitumia vibaya unavuruga utaratibu. Ndio mana usipoona vile
ulivyonavyo kwenye fikra zako utapata shida. Kila alichokupa Mungu kina thamani
ila fikra zako ndio huondoa thamani yake.
Yesu alipowaambia nileteeni
hapa wale wanafunzi wake alikuwa anamaanisha peleka kwake kwa njia ya Maombi.
Chochote ulichonacho au unachoona hakina thamani kwako mletee kwake. Kubariki
ni kuvipa nguvu ili vifanikiwe. "To Empower and Prosper". Mfano,Isaka
wa baada ya kupelekwa madhabahuni alikuwa ni tofauti na Isaka wa kabla ya kupelekwa
madhabahuni. Alipopelekwa madhabahuni fikra zake ghafla zikapanuka na kuona
possibilities
Chochote ambacho hakiendi
mpelekee Yesu kwa njia ya maombi. Mwili wako ukiuweka kwenye madhabahu ya Bwana
huwa unageuzwa nia. Mungu ana mipango mikubwa kuliko gari unayotembelea. Ana
mipango mikubwa kuliko chochote ulichonacho. Ndio maana ni vizuri kuweka akili
zako kwa Bwana.
Funzo la Tano
Ukomo wa kufikiri kwako
kusizuie kiwango cha utii wako katika kutekeleza wazo ulilipewa na Mungu
2Wafalme 4:6
Ikawa, vilipokwisha kujaa
vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena
chombo. Mafuta yakakoma.
Mwisho wa kufikiri kwa mama
mjane lilikuwa ndio mwisho wa mafuta kupatikana. Thamani ya mafuta haikuwa
kwenye mafuta bali kwenye fikra zake. Vyombo alivyoleta kwa mtumishi Elisha
ndio ukawa mwisho wa kupatikana kwa mafuta. Unapomuwekea Mungu mipaka
unajiwekewa mipaka wewe mwenyewe. Hii ni muhimu. Mungu hukuletea Neno na Roho
wake vikusaidie lkn utekelezaji wa akili (fikra zako) huwa una maana sana kwenye utekelezaji wa
namna Mungu anavyokusaidia.
Fundi akiharibu kitambaa
chako cha suti thamani ya Fundi ipo kwenye;
1. Kusikiliza vizuri
2. Kufikisha ukomo wa namna
anavyopaswa kukitumia kitambaa.
Wengi wanaishi maisha
"substandard." Wanapopata maisha ya mtumba "wanaridhika".
Lkn Mungu ana maisha mapya anayotaka uwe nayo. Fikra zako ndio mwisho wako.
Suleiman alipomjengea MUNGU nyumba aliijenga vizuri sana na kabla Mungu hajaingia aliridhika nayo
kwanza.
Kwanini unataka Mungu
aingilie maisha yako wakati ulivyojiweka mbele za Mungu ni kiholela holela tu.
Haiwezekani. Ukishinda vita kwenye fikra
utashinda maisha kwenye mwili. Kiongozi yoyote ni lazima awe trained fikra
zake. Uongozi sio cheo ni mtazamo wa kifikra. Pressure ikija fikra zitakuumbua
kwakuwa huna utulivu wa fikra. Ni lazima
ujiweke kwenye madhabahu ya Bwana usafishwe. Mungu atakupa akili kwakuwa
alikuumba yeye.
Mungu alipotuumba alitaka
tufike mbali sana .
Dhambi ikaharibu. Pata picha pamoja na dhambi zetu bado tunarusha madege
makubwa angani je kusingekuwa na dhambi tungefanya nini? Akili ni fursa. Unaona pale mwingine asipoona. Kuna fikra
nyingine hazioni kesho. Zipeleke fikra kwenye madhabahu ya Bwana. Naye atafanya.
No comments:
Post a Comment