HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA
FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA
➡Tumeshaangalia hatua 2 tuko tumeanza seminar. Leo
tuendelee na ya 3
3⃣Panga FIKRA zako kwa upya ili zisikupitishe tena
mahali pabaya ulipokwisha pitia.
✅FIKRA zinapangika
✅Mfano kwa mama mjane baada ya kusaidiwa na Elisha
akitaka hali ile ya mwanzo isijirudie tena lazima abadiri kufikiri kwake la
sivyo ile hali atarudi tu
2Falm 5:7
Mama mjane alipanga FIKRA
zake kwa upya..lazima ujifunze kupanga FIKRA zako kwa upya
Tuonaona mstari wa 7
➡...Nenda kauze mafuta...
Si FIKRA tu kutumika bali
MUNGU alitaka Mama mjane ajuaje na akubali ndani yake kuwa MUNGU ndiye
amfundishaye kupata faida.
Isy 48:17
✅MUNGU hakufunsidhi tu kuhubiri au kuimba bali pia
ukufundisha na upanga FIKRA zako ili zipate kujua MUNGU ndiye akupaye faida
✅FIKRA lazima zipate msaada wa kufundishwa jinsi ya
kupata faida
✅Pata tofauti sana
kati ya kufundishwa kupata faida na kufundishwa Biashara. Ni sawa na ilivyo
tofauti kati ya kufundishwa kufaulu mtihani darasani na kufundishwa juu ya
kufaulu mtihani wa kimaisha
✅Maana si kila mtu aliyeko darasani atafaulu maisha, na
si kila afanyaye Biashara atapata faida..lazima ujifunze kuvuka hapa
MAENEO MUHIMU YA KUTAKIWA
KUBADILIKA
1). Weka FIKRA zako zikubali
MUNGU ndiye anayekufundisha kupata faida
▶Watu wengi wakikwama kiroho ukimbilia kanisani ila
uchumi wao ukikwama huwaoni kanisani ukimbilia Benki, sasa sisemi Benki ni
mbaya au usiende Benki ila wanasahau kuwa
▶ROHO MTAKATIFU ni mwalimu mzuri sana wa kukugundisha ujasiriamali wenye
kupata faida
2). Lipa Deni
✅Elisha alimwambia Mama mjane ....kauze kisha lipa
deni....
✅Alikuwa anatafuta kitu gani?
▶Alikuwa anapandikiza nidhamu za kutumia fedha ambazo
MUNGU amekupa kwa sababu zake alizokupa au ulizomwomba tena kwa mwongozo wake!
▶Mama mjane alikwenda kutaka msaada wa watoto wake
kitokuchukuliwa watumwa(Alitaka kupata fedha za kuwakomboa watoto wake)
▶Hakuwa na FIKRA zilizojengeka kulipa deni maana Biblia
haituonyeshi aliwahi kukopa. Kama huna FIKRA
za kukopa huwezi ukawa na FIKRA za kulipa deni.
Mama mjane alikabidhiwa
matumizi ya fedha ktk maeneo haya
⚫Kulipa deni
⚫Gharama za kwake na zile za baadaye
⚫Gharama za watoto na za wakati ule wa baadaye
⚫Kuhakikisha ya kwamba amalizi faida lazima abaki na
mtaji.
✳Je unamwomba MUNGU pesa kwa ajili ya nini au kwa ajili
gani?
▶Kumbuka pesa uyumbisha mawazo na kujikuta watumia nje
ya lile kusudio
▶Ukikorofisha hapo MUNGU ukaa pembeni. FIKRA zinahitaji
nidhamu kwenye matumizi ya pesa. Kama MUNGU anakupa kwa ajili ya kitu fulani
hakikisha unaielekezea hyo pesa kwenye hicho kitu.
▶Tofauti na hapo utaona ROHO MTAKATIFU anakuhimiza TOBA
Mith 13:22
▶Watu wengi wana FIKRA za kujitazama wenyewe tu kwenye
upande wa pesa wanajikuta kusahau kuwa wana familia na watoto!
▶Biblia inatuhimiza kuweka akiba mpaka za wajukuu!
▶Usitazame kukwama kwa mme/mke wako ama wazazi wako,
usifike mahali hata pa kuwakasirikia badili FIKRA zako ili wewe uvuke hapo
kisha mrushie kamba naye atoke hapo oooh hallelujah Hallelujah
HOME WORK
➡Orodhesha madeni yako
Zab 37:21
✳Umuhimu wa kuorodhesha madeni
▶Usipolipa mikopo MUNGU haji kukupigania katika haki
zako.
▶Unapoteza haki katika haki
▶Mikopo isiyolipwa ugeuka deni
▶Deni ubeba vitu (rehani) ili akili zako ziamke. Na
baada ya kutaka kuja kuvichukua ndipo akili zako zitaamka
▶Si kila ambaye anashindwa kulipa deni hana hela bali
hana mpangilio mzuri wa matumizi na ulipaji
Yer 22:21
✅Si kwamba hapendi kusikia bali hataki kusikia maana
yake hataki kutekeleza alichoambiwa
✅Gharama kubwa ya kutokufaulu mipango yako ni kupoteza
utulivu wa MUNGU kukusemesha
✅Wengi wakisha kopa kwenye kulipa ulipa nusu na nusu
wanaweka mfukoni wanasahau MUNGU ndiye aliwafundisha kupata faida na au
walipewa kibali cha kupata mkopo
✅Usije ukasahau na kusema huu utajiri ni nguvu zangu
wakati ni MUNGU ndiye aliyekupa nguvu za kupata utajiri
No comments:
Post a Comment