Thursday, January 4, 2018

SISI NI WASHINDI ILA TUPO KATIKA VITA


Kwaiyo kama sisi ni wenyeji katika ufalme wa Mungu inabidi tujue kuwa Mungu anatujali  (God care us)

Lakini shetani apendi tuwe na furaha  na apendi tukae katika uwepo wa Mungu apendi tuwe wenyeji katika familia ya ufalme wa Mungu kwa kuwa anawivu na anajua furaha ya mbinguni ilivyo. Kwa kuwa alikuwapo zamani mbinguni akamuasi Mungu BABA. 

Kwa hiyo shetani anafanya kila hali atudanganye sisi  (Yohana 8:44) .
Tena mtu kabla hajaokoka anakuwa utumwani yaani anakuwa kwenye vifungo vya shetani.  Lakini ashukuliwe Yesu kristo wa Nazareti ...ooooh HALELUYA!  kwa kuwa kupitia Yeye tumekombolewa pale msalabani 

Maana nyingine Yeye alitununua kwa damu yake ya thamani . Kwaiyo sisi ni wa thamani sana mbele zake. Na kila wakati anatujali.
Tutazame silaha tutakazo tumia katika vita.
Silaha hizi tunazipata katika EFESO 6:14-19,:

1. KUVAA KWELI VIUNONI MWETU .

Kweli ni Neno la Mungu Na Neno la Mungu linabidi likae ndani yetu kila itwapo Leo.  Kwa Maana katika Neno la Mungu kuna utakaso Na umilikishwaji (Yohana 17:17)  Tena Mungu huangalia Neno lake apate kulitimiza.
Pia katika Kweli tunawekwa Huru  (hii ina Maana kuwa utapokuwa Na Neno ndani ya Moyo wako au Mwilini mwako  kuna vifungo vinachilia katika maisha yako kama Magonjwa.huzuni. nk. ) Vinatoweka kabisa  (Yohana 8:32)

2. TUWE WENYE HAKI.

Hapa tunatakiwa katika maisha yetu tuwatendee mema walio tuzunguka katika shughuli zozote.  Kimwili Na kiroho ili Yesu atukuzwe kupitia sisi. (1 thetholonike 1:8)

3. KUFUNGIWA MIGUU YA UTAYARI WA IMANI

Pale unapo hubiri Habari njema za Yesu kristo unatangaza amani Na wokovu ambao unaleta hiyo amani. Ili walio vunjika Moyo wapate kupona,  wenye huzuni wapate furaha. ..ili watu wakumbuke Yupo Mungu anae tupenda. ..kwa maneno mengine kuhubiri injili ni kutangaza Pendo la Mungu kwa wanadamu. .(isaya 52:7)

4. NGAO YA IMANI NA CHEPEO YA WOKOVU. 

Tunatakiwa tumpinge shetani kwa imani dhabiti. ..Pia inabidi tuwe Na imani kubwa ili tuweze kupigana vita vizuri  (1 petrol 5:9)
Ili tuweze kuushinda ulimwengu inabidi tuwe Na imani kwenye jina la Yesu kristo Na tuujali wokovu tulioupata  (Ebrania 2:3)

5. UPANGA WA ROHO 

Likiwapo Neno la Mungu ndani ya Moyo wako halikai bure bali lina badili maisha yako na kufanya uponyaji ndani ya Mwili wako. Maana linakuwa hai yaani linaishi na kutawala maisha yako kupitia Roho mtakatifu. Ndo mana biblia inasema Neno la Mungu Li Hai na lina  Nguvu. .HALELUYA!
(Ebrania 4:12,yeremia 23:29)

No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...