Saturday, December 22, 2018

KIONGOZI


 

                             YEREMIAH 1:5

Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Uongozi na usimamizi ni kitu ambacho wote tunatakiwa kujua na kuelewa, kwako kinaweza kuwa kipya au ulishawahi kwenda  ulifanikiwa kujifunza kwenye taasisi au chuoni.
Kila  mtu amezaliwa kuwa kiongozi na tunatakiwa kutumia skills hii katika kazi zetu na tuwajibike iwe kanisani au katika jamii au hata nyumbani
Kama unataka kuwa msimamizi au kiongozi mzuri ni vema uanze kufanya kwa vitendo katika shughuli zako za kila siku iwe nyumbani au katika shughuli za kawaida.

·       Kiongozi huwa anaonesha uelekeo na ku inspire timu kufanya kazi ili wafikie lengo husika, kumbuka kiongozi lazima kila siku awe anajifunza

·       Hakikisha kila mtu unaemuongoza  ajue mawazo yako na kuamini kuwa hicho kitu unachowaongoza kitafanikiwa

·       Pia tengeneza wingu la furaha katika mazingira mnayofanyia kazi ili kila unaemuongoza  ajisikie kuwa ana thamani.changamoto ikitokea jitahidi kuwa fear kwa kila mfanyakazi.

·       Changamoto ikitokea wewe ndo uwajibike , usijalibu kumlaumu mtu unaye moungoza zaidi unatakiwa kumkumbusha ni kitu gani afanye na ikibidi muonye kwa upole.

·       Pia jitahidi kujenga team work yenye nguvu katika watu wako na ushirikiano mzuri.ili kama kuna mapungufu ,watu unaowaongoza waweze kukusaidia kimawazo na kuafanya kazi kwa moyo wa kupenda.

BIBLIA INASEMAJE?

Kiongozi lazima uwe una hofu ya Mungu ili kuongoza watu katika maadili mema, hakikisha unaongoza sawasawa na mpango wa Mungu ili uweze kupata kibali mbele za wanadamu na Mungu mwenyewe

Kumbuka katika uongozi, kiongozi wako mkuu ni Mungu mwenyewe,  usiogope wanadamu  maana si kila mwanadamu anapenda umuongoze isaya 41:10

Kinachoitajika katika uongozi wako ni kujinyenyekesha kwa Bwana,unatakiwa ujue kila siku kuwa Mungu ndiye amekuweka  mahali hapo ili atukuzwe kupitiwa wewe, kwa kuwa amekuchagua kama mtumishi wake jua atazidi kukuinua juu kila itwapo leo.

Sawa tunaweza kuwa watumishi wa Mungu katika uongozi lakini tunatakiwa tuwe na bidii katika kazi zetu
Tufanye kazi tukijua kwamba sisi tuwabalozi wa YESU . Mithali 22:29

Kumbuka kiongozi ni mfano kwa wengine . mkabidhi Bwana njia zako pia umtumaini naye atakuafanya uwe kiongozi BORA.

No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...