Thursday, January 10, 2019

FURAHA YA BWANA NI NGUVU KWAKO



  



                            ZABURI 29:11 unasema...

Bwana atawapa watu wake nguvu, Bwana atawabariki watu wake kwa amani.

Binadamu kuna wakati tunafika tunachoka  kimwili na kiakili kwasababu kuna force ambayo tunatumia kwenye shughuli flani kwaiyo inafika wakati tunachoka. 

 MFANO WA KUCHOKA KWA JINSI YA KIROHO

Kwa jinsi ya rohoni kuna mstari kwenye biblia unaniambia kuwa  tunafanywa upya siku hadi siku (2 corinthians 4:16).. hii inatukumbusha kuwa kuna wakati roho   inachoka kufanya kusudi la Mungu.. na ndomaana tunatakiwa tujifunze mambo mengi ya rohoni ili tuwe na uzoefu…tujaze mioyo yetu neno la Mungu. Ambalo linatusaidia  kujua vitu vya rohoni… na linatusaidia kutia nguvu roho zetu ili tusichoke kuipigania imani. Mungu akitaka kupitisha vitu anapitishia rohoni afu vina be transformed kwenye ulimwengu wa kawaida.

MFANO WA KUCHOKA KWA JINSI YA MWILINI

Kwa jinsi ya mwilini kuna mstari kwenye biblia unasema kusoma sana kunauchosha mwili (Ecclesiastes 12:12)   pia kuna sehemu tunaona Yesu alichoka akakaa kalibu na kisima (John 4:6) hii inaonesha kuwa kuna wakati kwa jinsi ya mwili kama wanadamu tunachoka.. atuwezi pekee yetu tunahitaji msaada wa Mungu. Kuna wakati unatamani kusoma vitabu lakini kila unapogusa kitabu unahisi umechoka na unatamani ulale, sikia Mungu anakuwazia mema … Mungu anataka aanze na kukutengeneza rohoni kwanza afu aje mwilini … ukikaa vizuri rohoni  utakuwa na uwezo wa kuu control mwili wako .

Kuna wakati flani unafika mtu anakosa nguvu ya kuomba anatamani apate nafasi ya kuomba lakini anashindwa
Kuna wakati mtu anafika anatamani asome Neno la Mungu lakini anajikuta anashindwa

Kuna wakati mtu anafika anatamani afikie malengo ya mafanikio katika uchumi lakini anashindwa

Na kuna wakati mwanafunzi anatamani apate nguvu ya kusoma ili aweze kufaulu zaidi lakini anajikuta anashindwa

Rafiki hiyo hali ipo kwa kila mwanadamu hata wanafunzi wake Yesu walishindwa kuomba na Yesu angalau lisaa limoja..sio kwamba hawakupenda  laikini walikuwa hawana nguvu ndani yao
Jibu ni kukaa kalibu na Mungu na kumuomba akutie nguvu ili uweze kufika hatua flani.

Tatizo sio wewe tatizo ni shetani ambaye humfanya mtu achoke ili huyo mtu asiweze kusonga mbele na kushindania imani.

Naupenda huu mstali  nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu
(Philippians 4:13) kumbe yupo awezaye kututia nguvu katika kila changamoto tunayo pitia ,ambaye ni YESU KRISTO WA NAZARETI kwa maana atujua ni ya mioyo yetu. Anajua kuwa tunataka tuvuke daraja flani ilitufanikiwe lakini anasubiri uje usemezane naye uwe kalibu yake . tena anasema kuwa Yeye alituchagua sisi tuwe wake na tena ametununua kwa damu ya thamani  kwanini asitutie nguvu kwasababu tumezifuata njia zetu wenyewe tumemsahau yeye . 

Napenda huu mstali Huwapa nguvu wazimiao humuongeza nguvu yeye asiye na uwezo           (Isaiah 40:29) kwaiyo yeye Bwana atujua tulivyo tukimkalibia atatusaidia.

Naweza kusema kuwa Yesu ni Bwana wa viumbe vyote na tena ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote  kwaiyo kama yeye ni bwana wa viumbe vyote.. nadiriki kusema nguvu za aina yoyote zinamjua udhaifu wowote unamfahamu kwa kuwa alikuwepo kabla ya misingi ya dunia kuwekwa.  yeye ni Bwana wa milele tena hazimii wala achoki  akili zake azichuruziki..

Wewe usiekuwa na uwezo  ujue na ukili kuwa yeye ni Bwana wa vyote  katika eneo ambalo unakosa nguvu muweke yeye naye atafanya jambo katika maisha yako.

Napenda mstari huu kwa ulivyotafsirika kingereza My soul is weary with sorrow, strengthen me according to your word
Kuna wakati nafsi zetu zinakuwa hazina hamu wala uzito wa kumtafuta Bwana, lakini tumeruhusiwa kumwambia Bwana vile tunavyojiona kwamba KUPITIA NENO LAKO NAOMBA NGUVU.

Ujue  Mungu wetu  ni Mungu mwema hata kama umetenda dhambi kiasi gani, au dhambi zako zijakuwa nyekundu kama damu yeye ni mwaminifu anasamehe na kusahau kabisa na kukutia nguvu ya kuishinda dhambi.

Mwisho naweza kusema kwamba  majira haya na nyakati hizi ni za kuishi na Yesu kwa maana Neema ingaliipo katikati yetu katika
 Nehemiah 8:10 bible says that go and enjoy choice food and sweet drinks, and send some to those who have nothing prepared. This day is Holy to our Lord. Do not grieve, for the joy of the Lord is your strength.

 kumbe furaha ya Bwana ni nguvu kwetu Basi ilituwe na nguvu ni kufata sheria zake ili tumfanye atufurahie .. kwa maana akifurahi. Bwana anataka tutende yaliyo mema kamwe awezi kukuacha uangaike atakuapa nguvu za kukupa utajiri kwa maana haijawahi kutokea mwenye haki akaachwa na wala watoto wake kulanda barabarani Mungu anajua tunapopitia na tena anatuwazia mema anatamani tusogee kwake tutengeneze urafiki nay eye atatutia nguvu kwenye kila kitu. AMEN

No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...