Bila kuwa na Imani binadamu hatuwezi kupata ukombozi,
ukisoma katika waebrania 11:1 inatueleza kuwa basi Imani ni kuwa na uwakika wa
mambo yatarajiwayo, ni bayana na mambo yasiyoonekana.
Pia tunasoma katika (wakorintho 5 :7) biblia iantuambia kuwa maana twaenenda kwa Imani, si kwa kuona, kwaiyo naweza sema kuwa ukombozi wa mwanadamu unaanzia ndani. Yaani utu wa ndani/ moyoni. Maana hata Mungu huangalia moyo,
(1samwel 16:7) 7 Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.
yeye haangalia kama sisi wanadamu kwa macho ya nyama, na hata Mungu akitaka kukujibu maombi yako mchakato wote uanfanywa katika utu wako wa ndani ndipo transformation inafanyika kuja kwa jinsi ya mwili. Mwanadamu ukiwa vizuri kwenye mambo ya rohoni automatical unakuwa connected na Mungu kwa sababu network ya mawasiliano yenu yanakuwa mazuri,
Kwa maana (warumi 10:9-12) inaeleza kuwa kwa sababu,
ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini
hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Kwaiyo tunaona kuwa kuamini kunaanzia moyoni lakini
pia unatakiwa kile unacho amini ukitamke kwa sauti yaani kwa kinywa ili kiumbike
kwa jinsi ya mwili.
25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila;30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
Katika vifungu hivyo inaongelea kuhusu Paulo na sila,
walipotupwa gerezani, story inatueleza kuwa katika usiku huo walikuwa wakiomba
na kumwimbia Mungu nyimbo za kumsifu, yaani walikuwa wana mtukuza Mungu ghafla pakawa na tetemeko kuu la nchi
hata misingi ya gereza ikatikisika, tunaona mlinzi wa gereza alishangaa yaliyotokea
akaogopa akataka kujiuwa. Alishangaa na kuogopa aliyo yaona akauliza Bwana zangu,
yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?paulo na sila wakamjibu MWAMINI
BWANA YESU , mpendwa tunacho
takiwa ni kumwani Bwana Yesu kwa kila kazi alizofanya na kuamini kupitia yeye
dunia iliokolewa, maana yeye alikufa msalabani kwa ajili yangu mimi na wewe ili
tuweze kuishi Maisha ya ushindi hapa duniani.
Yamkini
unapita Maisha magumu, nikutie moyo tu ukimwamini Yesu naye hatokuacha uangamie,
tena yuko mlangoni mwa moyo wako anabisha hodi, anasema katika....
ufunuo 3:20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti
yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye
pamoja nami.
Yesu anatuambia kuwa tukisikia sauti yake na kufungua mioyo yetu aingie ndani
yetu, tutakula pamoja nae, hapa anamaana kwamba tutaweza kuzungumza nae na kupeana
habari za furaha, anaposema atakula na sisi anamaana hawezi ondoka upesi, ataumega
mkate kama kwa wale wanafunzi wa Emmausi ( luka 24:13-35), atakaa na sisi na
kutujulisha jinsi ya kupata itaji letu kama alivyowaambia wakina petro pale
walipokosa samaki usiku kucha (9 YOHANA 20:1-13), atatupa baraka na kuondoa
mapungufu yetu, shida zetu, magojwa yetu.
Yamkini unasumbuliwa na ulevi mwamini Yesu
una umruhusu utapona, yamkini uanteswa na madawa ya kulevya mwamini yesu utapona. Hakuna mtu alienda
kwakwe akatoka bure. Yote kwakwe yanawezekana.
Katika hali hiyohiyo mwamini yesu naye atakusaidia .
Paulo na sila
walimwamini mungu katika shida yao, walifungwa mikatare, ndani ya gereza lakini
walimuamini yesu, sijui gereza lako ni lipi lakini nina neno moja kwako mwamini
YESU, sijui una mikatare gani Maisha mwako yupo Yesu mnazarayo atakufungua
ukimwamini…
Hawa watumishi walimtukuza Mungu wakati wa shida,
wakati wanauguza majeraha ya mapigo, wanatufundisha kuwa haijalishi unapita
katika hali gani ya Maisha, haijalishi unapita katika nyakati gani za Maisha ,
hajialishi unapita katika majaribu ya namna gani, tunatakiwa tumtukuze Mungu
alie hai, kwa maana katika sifa Mungu anashuka, katika Maombi Mungu husikia
kilio chetu.
Labda unaweza kusema Maisha yako unapitia katika giza
nene ambalo uwezi kuona Maisha yako ya mbele, nikuambie tu mpendwa kuwa usiache
kuomba , usiache kumsifu Mungu maana hata wakina Paulo na sila walikuwa katika
giza hilo, hawakujua hatima yao ya Maisha ya kesho, walichokuwa wanajua kuwa Yesu
ni Bwana.
Yamkini ndugu na marafiki zako uliokuwa nao katika dhiki hiyo wamekata tamaa
wanakushangaa na kusema na kutazama jinsi unavyo mtukuza Mungu na kuomba ,
usiwasikilize ,usiwatazame, wewe mtukuze Mungu kwa maana hata wakina Paulo na
sila wenzao gerezani waliwashangaa hivyo hivyo. Mpaka Bwana aliposhuka
kuwakomboa.
UNATAKA KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA
YAKO ? NA JE LABDA ULIANGUKA KATIKA
DHAMBI UNATAKA KUTENGENEZA NA YESU, FUATISHA SALA HII
BWANA YESU NAKUALIKA KATIKA MOYO WANGU,
NATUBU DHAMBI ZANGU, NAOMBA UNISAMEHE, NIMEKUKOSEA SANA LAKINI LEO NAFUNGUA
MOYO WANGU PIA NASEMA NDIYO KWAKO, NAKUALIKA UWE BWANA WANGU NA MWOKOZI WANGU
KWA KUWA WEWE ULIFUFUKA NA MIMI UMENIFUFUA, KWA JINA LAKO YESU KRISTO AMEN…
FURAHIA MAISHA YA USHINDI…..

No comments:
Post a Comment