Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.
Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.
Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.
Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.
YOSHUA. 1:3-6
Kwa wale waliozaliwa katika agano, uzao uteule watu wa milki ya Mungu watu walio okoka . Wanao mwamini Yesu kuwa Bwana na mokozi wa maisha yao.
Watu wenye kuishindania imani... Mungu amewapa kutawala kila eneo la ardhi wanapo kanyaga. Ila kama unajua kuomba jinsi ya kujiunganisha na ardhi.. na kuomba toba juu ya ardhi ili uweze kupata baraka zilizo kwenye ardhi hiyo.
Haijalishi ardhi hiyo iko katika hali gani. Unachotakiwa kujua kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu na unayo mamlaka ya kiagano na muumba wa Mbigu na nchi..
Na hii inatukumbusha kuwa kuombea ardhi ya mkoa unao ishi.... au ardhi unayokaa ili baraka zifatane nawe kila uendako. Na kufanya toba ....
Pia tunatakiwa kuwa na moyo wa ushujaa kwa kila kazi iliyo kuwa mbele yetu... ujasiri ndio utakao tufanya kugundulika kuwa sisi ni wana wa Mungu...
Tumepewa Moyo wa ushujaa si kwa ajili ya kujihami bali kwa ajili ya watu wanao tuzunguka .. kuanzia ndugu hadi jamii nzima.. kuna wakati wanaitaji msaada wa ki fikra, maombi, uchumi, furaha.. kama tusipokuwa na ujasiri wa kusonga mbele basi kazi iliyotuleta hapa duniani hatujaifanya...
Mungu ameapa kwamba hatokuacha...zaidi tambua nafasi yako katika jamii...
AMEN
No comments:
Post a Comment