Wakati kama huu ni wakati wa kung'ang'ana na Yesu na kulisoma Neno lake ili tuweze kusikia atakoacho tuambia, shetani akileta sauti ya hofu atuwezi kuisikia maana masikio Yetu yapo kusikia sauti ya mchungaji mwema Yesu...
Kwaiyo wale wampendao watajitahidi sana kusoma Neno lake na kufanya maombi kwa kwa jinsi ya mapenzi yake.
Lakini pia watatamani malisho yake yaani Neno lake lisiwapite wakati wote na Muda wote... kama jinsi unavyokula chakula cha asubuhi, mchana na jioni..
Mwili unaitaji chakula ili uweze kutengeneza nguvu mwilini , lakini pia roho inaitaji chakula kama mwili ili iweze kusimama katika imani,
Kwaiyo tukiwa na Yesu na akitupa chakula chake kila siku, imani Yetu inajengeka na tutakuwa imara siku hadi siku, tutapanda imani hata imani, utukufu hadi utukufu.
Katika nyakati zote za njaa, ziki, utumwa, hata za magonjwa tusome Neno la Mungu ...
See 👉 Yohana 10 : 4.
#covid19, #Goodnews,
No comments:
Post a Comment