Wednesday, March 24, 2021

MAOMBI YASIO YA UBINAFSI

Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
Yak  ‬15‭-‬16 

Biblia inatufundisha vitu 3
1. Toba
2. Maombi
3.bidii

Toba
Tunafundishwa kuwa tukumbuke kuomba toba kwa ajili ya yetu na wenzetu,
Watu wengi wakienda mbele za Mungu hawakumbuki kuomba toba kwa ajili ya wengine..... ,  na hii hupelekea maombi yao kutojaa majibu yanayostahili katika kuomba kwao. 

Tunaomba toba si kwamba tumetoka kufanya dhambi ,hapana bali unapoenda mbele za Mungu  lazima ujitakase kwa maana yeye ametukuka, pia sisi sio wakamilifu kwaiyo tunaitaji damu ya Yesu ili tuweze kufika katika ukamilifu wa Mungu. 

2. Maombi

Watu wengi tunapoenda kuomba huwa tunaenda kwa ajili ya maendeleo yetu na sio maendeleo ya wenzetu .

 Tunaona kuwa Yesu alituombea sana kuliko kujiombea yeye, hapa anatufundisha kuwa mpende jirani yako kama nafsi yako,  na hii ndio huduma ambayo Mungu anataka , maana alisema anatafuta mtu katika nchi ili alijenge boma, yaani sehemu iliyobomoka , kubomoka wapi sio kwake huyo mtu bali taifa,kanisa ,familia ,jamii .... 

3. Bidii

Lakini tunaona kuwa biblia inatufundisha kuwa kuomba kwa mwenye haki kwafaa kuomba kwa bidii, kwaiyo tunatakiwa tuwe watu wa kuomba sana na kwa ufasaha, 
To be continue......

No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...