.
Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.
Kuna watoto ambao wamezaliwa kwa ajili ya kufanya kusudi la Mungu , wengine wanatimiza maono ya babu zao, au wazazi wao.
Wengine wana malizia huduma iliyo anzishwa na ndugu zao, na wengine wanaweka msingi wa huduma kwa ajili ya kizazi chake kitakacho kuja,
Anaweza asiwe mtoto wako wa kumzaa lakini anapenda kile kitu ulicho nacho, kama wewe mhubiri na yeye anatamani kuwa ni mhubiri, kama mwimbaji anaweza kutamani kuwa mwimbaji, hawa wote tunaita ni watoto,
GAL. 4:19-20 SUV
Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu; laiti ningekuwapo pamoja nanyi sasa, na kuigeuza sauti yangu! Maana naona shaka kwa ajili yenu.
Paulo anatujulisha kuwa alikuwa na watoto ambao alikuwa anawashape ili kazi alioanza isiwe bure iwe kizazi hata kizazi, kwaiyo kazi ya Mungu haina hasara Mungu akikupa nafasi ya kuishi nyakati tofauti tofauti anakupa watoto ambao watabeba kilicho chako ili utakapo maliza safari yako , wawepo wengine wakuendeleza gurudumu.
EZE. 22:30 SUV
Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.
Kuna watu ambao hawajawahi waza kama nikifa au nikimaliza kazi, je nitamwachia nani? Hapa inaonekana katika hiyo nchi hakukuwa na mtumishi hata mmoja. Au walikuwepo wakafa na vitu vyao, hawakurisisha huduma kwa kizazi kingine...
Lakini pia
Mungu anatukumbusha kwenye mstari huu kuwa anatafuta mtu miongoni mwa watu ili aweze kusimama mbele zake na kuchukua vya kwake vidhihirishwe duniani. Unaweza ukasema kuwa nyumba yangu yoote wameokoka , au ukoo wangu woote wameokoka lakini hayupo hata mmoja ambae amebeba kazi ya Mungu.
Wapo wazazi ambao wanajua kuwa mtoto wake anakitu lakini anapuuzia . Kile kitu kitakuwepo lakini shetani akija anakiiba unakuta mtoto alianza vizuri kuimba kanisani baadae unakuta anaimba mapenzi, alikuwa mhubiri mzuri anakuwa MC unakuja alikuwa anakipawa cha kuomba unakuta anapenda kukaa sana kijiweni...
Inapelekea baadae kile kitu kinapoa, Mungu anasubiri miaka 25 baadae yule mtoto kakuwa naye anawatoto Mungu analudisha kipawa kwa mtoto wake .....
NINAKUOMBEA KWA JINA LA YESU KRISTO
Uwe productive katika huduma uliyopewa
Ujue kilicho ndani ya watoto wako na wajukuu wako
Mungu aseme na wewe kuhusu kurisisha huduma kwa wengine
Ukumbe kuwaombea na ufalme wa Mungu ukae ndani ya watoto wako
Kile ulichowapa watoto wako ukiombee mpaka kitakapo timia kwa wakati wake.
Part 2
Itaendelea......
See 👉 Yoshua 1 :6
No comments:
Post a Comment