Tuesday, October 5, 2021

MUNGU YUPO NA ANAKUSIKILIZA MAOMBI YAKO.

Isaya 41:21

Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.

Mungu anatupa nafasi sisi watoto wake tuweze kuongea kile kitu ambacho tunataka tufanye, tufanyiwe, kitokee au kisitokee.

 

Hoja zenye nguvu

Mungu anatupa ruhusa ya kujadiliana naye mambo yetu ambayo tunataka kumshilikisha.

Mungu anataka tutumie akili na moyo pale tunapo taka kusema naye,

Tunapoenda mbele za Mungu tutumie moyo ili tuweze kuweka Imani zetu kwa yeye ili tupate itaji letu.

Imani juu ya unacho kiomba basi utapokea.  

Ebrania 10 : 38

Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.

Imani inakaa mioyoni [ warumi 10 : 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu ]

 Isaya 1:18a

Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Kwenye biblia ya kingereza kasema come now let us settle the matter

Settle : to reach a decision or an agreement about something, or to end a disagreement:

Hapa bado Mungu anatusogeza  karibu, kwa njia ya kusolve tatizo , yaani kuyajenga, kuondoa tofauti zetu.

Mungu wetu alituumba akatupa uhuru wa kufanya jambo,

Tuko  tofauti na viumbe vingine, Ametupa nafasi sisi wanadamu wa kujielezea mbele zake na hii ndio maana ya upendo (uhuru)

Mathayo 7 :7

Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?
10 Au akiomba samaki, atampa nyoka?

Bado mungu anaonyesha ukaribu na wanadamu yakuwa  chochote tutapata ila tumuombe yeye.

Kuna vitu vitatu katika mstali huu

1.     Omba ( ask)

to put a question to someone, or to request an answer from someone

2.     Bisha  ( knock)

to repeatedly hit something, producing a noise:

3.     Tafuta  ( seek )

to try to find or get something, especially something that is not a physical object:


Tunao uwezo wa kumshawishi Mungu tukiwa na Hoja zenye nguvu.

 Mathayo 11:12

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

Kjv bible

12And from the days of John the Baptist until now the kingdom of heaven suffereth violence, and the violent take it by force.

Suffereth  means  with unwilling permission

Violent means using force to hurt or attack

Biblia inasema ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka

Anaposema ufalme wa mbinguni anamaanisha;-

1.     Vitu  vizuri vya mbinguni

2.     Mamlaka ya kutawala ya mbinguni

3.     Uhuru ambao uko mbinguni

4.     Amani iliyokuwa mbinguni

Kuupata kwa nguvu anamaanisha kuufanyika kazi mpaka upate,

Kuuteka

-      Anaposema kuuteka Anamaana hatupewi, ila tunachukua bila lidhaa, yaani hatukustahili kuwanacho ila tunakuwa nacho.

-      Hukustahili kupata kitu flani ila unakipata.

Nakuombea ifike level ambayo kuna kazi ulitakiwa kuikosa, kwakuwa unazo nguvu za rohoro uipate kwa jina la Yesu ”.

 

Mifano ya watu ambao walikuwa na hoja na nguvu ambazo zilibadili mambo yao.

 

Ibrahimu                 (Mwanzo 18:19-30

19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.
20 Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,
21 basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.
22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana.
23 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu?
24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo?
25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
26 Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.
28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano.
29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.
30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.

 

Musa                     (Kutoka 32:9-14

Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu
10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.
14 Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.

 

 

 

Mfalme Hezekia           (Isaya 38:2-6)

Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana,
akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.
Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema,
Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.
Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu.

 

Hannah                  (1 Samweli 1:14-20)

14 Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako.
15 Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana.
16 Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa.
17 Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.
18 Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena.
19 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka.
20 Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana.

 

 

Yabesi                     (1 Nyakati 4:9:10)

Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.
10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

Nakuombea yakuwa Mungu azidi kukufungulia Neema ya kuisikia sauti yake. AMEN

No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...