Thursday, November 11, 2021

HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU

Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini,

 Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli,

 nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Yn 8:31‭-‬32 SUV



Neno la Mungu  ni Lihai na ni pumzi ya Mungu  

hii inatufanya kujenga hoja kwamba Neno la Mungu ni roho ya Mungu kutokana na isaya 11 : 2

Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;

Hivyo basi kwa kadri unavyokaa ndani ya maneno ya Mungu , automatically  nafsi yako inajiconect na Neno la Mungu (roho saba za Mungu)

Hivyo basi unajikuta unapata ufahamu  ndani ya maisha Yako kwenye kila tatizo linalokusibu

Pia kama kuna vitu vilikuwa haviendi kwenye maisha yako unakuta vinaenda kwa sababu Neno la Mungu linakuwa linajiendesha ndani ya akili yako, mwili wako, roho yako, 

Neno la Mungu ni kama mfumo/mashine ambayo imeingia ndani ya Maisha yako ambayo inatatua matatizo kwa urahisi.

Unapofanya maombi ukisema imeandikwa... pale una active mashine nafsini mwako ambayo hiyo mashine ni Neno la Mungu. Unakuta maombi yako yanapata majibu na hapo ndipo Yesu anasema NA HIYO KWELI ITAKUWEKA HURU. 

ni maombi yangu majibu ya maombi yako yajibiwe kwa jina La Yesu kristo

No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...