Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti;
Yn 13:2
Biblia inaambia kuwa Yuda alikwisha wekewa roho ya usaliti. Kwaiyo usaliti hauji tu kwa mtu kupenda ila ni kazi ya shetani. Na hii inatokana na kumwachia shetani mlango wa moyo wako.
Tunaitaji sana kuliweka neno la kristo katika moyo wetu ili mharibu ajapo jalibu kuingiza chuki ndani ya moyo wetu akute kumejaa Neno la uzima.
Yesu alikuja duniani ili tuwe na uzima tele. Uzima tele alikuwa na maana katika kila kitu ufanikiwe na kuonekane wema wa Mungu . Moyo wa mwanadamu umeumbiwa amani kufurahi na kupokea yaliyo mema kutoa yaliyo mema.
Kwaiyo unapo mpokea Yesu kuwa Bwana na mokozi wa maisha yako anakuletea uzima ndani ya moyo wako. Ndo maana watu wengi wanaojazwa Neno la uzima katika mioyo yao wanakuwa na amani siku zote.
Tafuta watu wanaoenda kanisani na mizigo ya maisha . Wakitoka tu kanisani wanakuwa ni wepesi kwa sababu ya Nenola uzima wanalopokea kwa makuhani wao.
Kwaiyo tunaitaji sana kumkimbilia Yesu kristo ili shetani asituingizie roho za giza. Kwa maana kama aliweza kumdanganya eva anaweza kukudanganya na wewe kama aliweza kumdanganya yuda anaweza kukudanganya nawewe.
Nakuombea kwa Jina la Yesu kristo wa Nazareth Roho mtakatifu akulinde na azidi kukuongoza katika njia ya imaniili shetani asiwe mdanganyifu
AMEN.
No comments:
Post a Comment