Monday, November 17, 2025

HAPO SIO SEHEMU YA KUPUMZIKA

 Mika 2:10 BHN
[10] Inukeni mwende zenu! Hapa hamna tena pa kupumzika! Kwa utovu wenu wa uaminifu maangamizi makubwa yanawangojea!


Kuna hali katika maisha ya vijana ambayo inamfanya mtu kurizika kiwango alicho nacho. 

Si vibaya , lakini biblia inatukumbusha kuwa katika hali yoyote ya mafanikio hatutakiwi kurizika wala kupumzika...

Duniani tunapita lakini pia tuna assignment kubwa ya kufanya   
1. Ufalme wa Mungu 
2. Maisha ya kila siku 

Chochote kilicho chema , tunachopata au tunachotenda ni kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Na uzuri Yesu alisema tuende ulimwenguni kote kuhubiri/kutangaza/kushuhudia mambo anayofanya kwenye maisha yetu .
Hiyo inaonesha kuwa hatutakiwi kupumzika maana tukipumzika tutadumaa kiroho, kiakili, na kimtazamo
Biblia ya NIV anasema

Micah 2:10 NIV
[10] Get up, go away! For this is not your resting place, because it is defiled, it is ruined, beyond all remedy.

Yesu anatamani kila siku tuwe na kazi ya kufanya kwa ajili ya ufalme wa Mungu. 

Kama kwenye biashara anatamani biashara iwe kubwa ili wateja waongezeke na washuhudie kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu 

Kama kwenye siasa , anatamani uwe kiongozi mkubwa sana ili Jina lake litambulike kupitia wewe

Kama ni ndoa , anatamani uwe mke au mume mzuri ili jamii iliyo kuzunguka waone maisha ya Yesu ndani Yenu.
Why wana wa Israel waliambiwa Na Mungu imetosha kuzunguka mlima ule 

Kum 2:3
Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha; geukeni upande wa kaskazini.

Kwa sababu anajua mwanadamu huwa anachoka na kudumaa akiwa sehemu moja...
So aliwaonyesha uelekeo ili wa Destiny yao ya maisha...

So Mungu akisema kuwa hiyo sio sehemu kupumzika kwako basi lazima akuonyeshe uelekeo wa kwenda.
Kuna nabii mmoja aliitwa eliya , malaika alimwamsha na kumpa chakula, na akamwambia ongeza chakula kwa sababu safari yako bado ni ndefu 

1 Kings 19:7 NIV
[7] The angel of the Lord came back a second time and touched him and said, “Get up and eat, for the journey is too much for you.”


1 Wafalme 19:7 SRUV
[7] Malaika wa BWANA akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako.
Kwa kawaida na akili zetu tunaweza sema tumefika lakini Mungu anasema bado safar ni ndefu..
Tunaitaji kuomba sana, kula neno la Mungu, kusoma , kujifunza hekima zote za dunia ambazo zitatusaidia kwenye maisha...

Yamkini hii safar yako ya maisha ni Ngumu lakini usikate tamaa, jiandae kwa ajili ya kizazi chako cha baadae.

Don't rest and don't give up...

Amen

No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...