UNAFIKIRI KWANINI MUNGU ALILETA SADAKA
▶Si kwamba ana shida na pesa yako
▶Lengo la kwanza lilikuwa kutumia sadaka kukutengenezea
FIKRA sahihi ndani yako
✳Tazama maana ya
⚫Malimbuko=MUNGU anataka umfikirie yeye kwanza
⚫Zaka ya kwanza=MUNGU anataka kupewa heshima ktk maisha
yako
✅Watu wengi kwenye kipindi kigumu na chenye kibano wako
tayari kutafuta hela kulipa Benki lakini si kwa MUNGU. Kwa MUNGU excuses
zitakuwa nyingi sana
na hata kusema "MUNGU we si unajua nilivyobanwa"
✅MUNGU hana maana wala hataki kukufirisi bali anataka
kukutengenezea FIKRA zenye Nidhamu
✅Jifunze kumpa MUNGU 100% naye anakurudishia 100%
✅Muulize MUNGU kwanza kwenye kila kitu, ratiba zako,
muda wako na mambo yako mkabidhi na mfikirie MUNGU kwanza
✅Usitamani kuiga maisha na FIKRA za mtu mwingine
hakikisha MUNGU anakupa mbinu za kujenga FIKRA za kwako mwenyewe.
✅FIKRA zenye kujenga nidhamu ndani yako.zitakufanya
utende haki wala hazitakupeleka kwenye kupokea rushwa
✅FIKRA hizi zitakuwekea unyenyekevu ndani yako,
kujishusha na kujifunza kutoka kwa wengine
✅Usijaribu ku copy na ku paste kutoka kwa mtu mwingine
BWANA atakupa mikakati sahihi ndani yako
HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA
FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA.....[Zinaendelea...]
2⃣Tasmini kufikiri kwako ili uweze kushirikiana na MUNGU
anapotaka kukusaidia kimaisha.
⚫Haifanani na hatua ya kwanza
⚫Tafsiri nyingine ni kama
ifuatavyo Mith 23:7
....aonavyo nafsini mwake...
➡Biblia haisemi aonacho bali aonavyo si afikiricho bali
afikirivyo si anachotafakari bali anavyotafakari
✅Kumbuka alichosema YESU kwenye Math 13:13-14
➡Biblia haizungumzi tu juu ya aonavyo, bali anaonavyo
anachoona
➡Kinachomsaidia kuona anachoona si swala la kufikiri
bali jinsi ya kufikiri
➡Ni kitu gani kinachokusukuma kufikiri na kuja na jibu
ulilonalo?
Kumbuka habari ya wale
wapelelezi 12
10:- waliona majitu
2:- waliona chakula
➡Walitazama lakini hawakuona
➡Ndivyo ilivyo wengi usoma NENO kumbe hawasomi, wengi
usikiliza kumbe hawasikilizi
⚫Shida ni nini??
➡Nafsi=FIKRA zimefungwa!
Rum 1:28
✅Ufahamu ulioko ktk nafsi ni tofauti na ufahamu ulioko
ktk roho
✅Unasema najuaje...ndiyo maana anazungumzia.habari za
akili hapa...na akili haipo rohoni bali kwenye nafsi
✅Ukimkataa MUNGU kwenye fahamu zako ama kumuacha, basi
utafuata akili zisizofaa, zako na za wengine!
✅Kwa sababu hyo utajikuta unafanya mambo usiyotaka
kufanya
✅Kwa lugha rahisi kumwacha MUNGU huwezi tembea ktk
mpango wake juu yako
✅Ukimkubali KRISTO hawezi kukuacha utembee nje ya
mpango wa MUNGU
Akili zisizofaa ni nini
Unachotakiwa wewe
kukijua/kukifuata wewe kama wewe!
Na wala si maana yake kwamba
ni akili mbaya❌
✅Maana yake ni FIKRA ambazo kwa mtu mwingine si zake
mwingine ni zake. Mfano mfanyabiashara astahili kumwona mfanyakazi ofisini
anafanya kisicho sawa na vivyohivyo mfanyakazi kumtazama mfanyabiashara kuwa
amepotea!
✅Ukiruhusu na kukubali MUNGU akutawalate anakupa FIKRA
za kusimama alipokusudia hata kama akikuletea
washauri watakushauri ktk FIKRA za MUNGU juu yako na wala hawatatumia akili
mbaya
✅MUNGU anataka kutusaidia ili tuishi maisha ya kiwango
cha Ki-Agano maana huko ndiko kwenye kusudi la kila mmoja!
✅Viwango vyetu vya maisha vimefungwa ktk Agano(kwa sasa
twatumia Agano jipya ila tusisahau na kuliacha maana ktk lile la kale MUNGU
alishaweka maagano pia)
Hebr 8:8-10
Hebr 4:12-13
➡MUNGU akitaka kukufanikisha utuma NENO ktk nafsi
yako(FIKRA) ili nafsi iweze kutafsiri lile NENO kati ya roho na mwili
➡MUNGU anapotuma NENO lile NENO lina uwezo wa kutambua
mawazo na makusudi ya nafsi
➡NENO ukagua aina ya FIKRA au mawazo uliyonayo ktk
kuendesha maisha yako.
Zab 117:19-20
✅Ukimlilia MUNGU utuma NENO lake na
NENO ukagua mambo haya:-
1⃣Aina ya FIKRA na akili unazotumia
2⃣Pia imsaidie maamuzi ndani yake aina gani ya
akili(FIKRA) unazihitaji mahali ulipo
3⃣NENO la MUNGU linampa MUNGU nafasi ya uhalali/kibali
kwako
Isaya 55:8-11
▶kuna pointi kama 4
hapa muhimu uzidake
WAZO:- MUNGU utuma wazo ndani
ya mtu
NJIA:- Ukisha tafakari wazo
ukupa njia(MIKAKATI)
MVUA:- Uachiliwa mvua kuzidi
kunyeshea listawi na kukua hilo
wazo
NENO:- kwa hiyo NENO
ufanikiwa hakika
➡Usishtuke litakapokuja wazo tofauti na ulilonalo hyo
ni ishara ya kuambiwa jipange ili utoke mahali ulipo
➡Kumbuka kama nafsi
yako haitakuwa tayari kupokea hata YESU asimame mbele yako utamgomea tu, sababu
ni nini mafundisho tunayopokea. Yoh 8:31-59
▶Ukikataa msaada wa maelekezo yake utakuwa na maisha ya
kuishi jangwani tu(maisha ya mzunguko tu usijue ushike nini uache nini) na
mbinguni ila jiulize Airport yako itakuwa wapi? Jangwani au Kaanani?
TURUDI KWA MAMA MJANE TUJIFUNZE KITU
2Falm 4:1-7
MASWALI AMBAYO YANAWEZA
KUKUSAIDIA KATIKA KUTATHIMINI KWAKO
1⃣Je ninajua ni aina gani ya masaada ninaohuitaji ili
niwe na maisha mazuri kuliko niliyonayo sasa?
✳Swali hili tunalipata kwa mama mjane baada ya
kujieleza Elisha akamuuliza swali nikufanyie nini
✳Mama hakujibu lile swali hakusema anahitaji msaada
gani bali alipekeka ripoti ya hali yake ya maisha aliyokuwa nayo baada ya kufa
mumewe.
✳Alishindwa kujibu yawezekana kwa mambo haya:-
-FIKRA zake hazikuwa na jibu
ya swali hilo
-FIKRA zake zilikuwa
zimeishiwa mawazo ya kumtoa ktk shida hyo
-FIKRA zake zilikuwa zinataka
kutua mzigo bila kujua atabebeshwa mzigo wa lile swali unataka nikufanyie nini
MUHIMU SANA KUFAHAMU SIRI ZILIZOKO KTK MASWALI YA
NAMNA HIYO
✳ Kushindwa kujibu maswali/swali la Elisha maana yake
au inaonyesha
✳Matatizo yake yalikula muda wake wa kufikiri kiasi
ambacho hakubakiza muda wa kufikiria jibu
✅Muda wako ukiliwa na kukatawaliwa na matatizo huwezi
fanya maamuzi, unapigwa bumbuazi huwezi pata hata wazo la kufanya ndani yako.
Utabaki kukaa na hasira na huzuni
✅Usikubali mazingira yakuwekee ngome
inayokwamisha/kuzuia kufikiri kwako zaidi ya mawazo uliyonayo sasa
Mwz 26:1-14
✳MUNGU aliisemesha FIKRA yake isitazame mazingira bali
aangalie Agano
2Kor 10:3-5
➡Shetani upambana na kuvuruga sana FIKRA ndani ya mtu
2Kor 11:3
✳Unapoona mapambano ya FIKRA ndani yako usiruhusu
kabisa matatizo kuyaona ni makubwa kuliko NENO ndani yako
✳Shetani uleta hila ndani ya mtu kwenye FIKRA ili
kukuvuruga
HILA MAANA YAKE NINI
1⃣Wazo linalokuja kukuzuia uwezo wa FIKRA zako kupokea
cha MUNGU na kama ulikuwa umekipokea
unakikataa
2⃣Ukweli+Uongo=Usipovitenga jibu ni Uongo. Jiulize pale
Edeni mti wa mema+mabaya=mabaya
✅Cheki wazo linapokuja ndani yako ROHO MTAKATIFU
anasemaje? Kama si la kusudi la MUNGU utakosa
amani, utapata huzuni(maana yake change your mindset fanya TOBA)
✅Uhitaji kufikiria mtu anayekuja na wazo fikiria na
sikia wazo la MUNGU pekee
✅Ukikosa amani usiendelee na hilo wazo
-Cheki ndoto unazoota kama ni
✳Nyoka=kuna hila inakuja kuvuruga FIKRA zako kama
kakung'ata ujue kaacha sumu na kama la jua
kaacha hofu!
✳Ngome=kuna kizuizi umefungiwa ndani, ulitakiwa kutoka
✳Stendi=Kufikiri kwako kumekwama
Unapoomba ombea sumu kuondoka
na kama kuna roho ya kufuatilia utekelezaji
bado ipo kemea
*Teka kila nyara na kila
FIKRA=zilizimishe kufikiri ki FLAME na KI AGANO
HOME WORK
✳YESU akisimama mbele yako leo akikusemesha unataka
nikufanyie nini utajibu nini??
✳Ukishindwa kujibu ni wazi kufikiri kwako kumekwama!
KWANINI MUNGU ANAULIZA MASWALI
HAYA
1⃣Kumlazimisha aliye uliza alazimishe FIKRA zake
kufikiri mahali zilipokwama
2⃣Anatafuta uhalali/kibali cha kuingilia kufikiri kwako
maana anaweza kuja na wazo jipya ukakataa
No comments:
Post a Comment