Kuna aina nyingi za kumshukuru za Mungu
1. Kabla ya kukupa kitu
2. Baada ya kukupa kitu
3. Umepata au hujapata
4. Umekosa vyote...
1. unaweza kupitia magumu kama ayubu . Mshukuru Mungu
akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
Ayubu 1:21
2.umepata kitu kwa uchache . Mshukuru Mungu
Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka.
Yohana 6:11
3. Umeponywa kama wakoma kumi , rudi kumshukuru mungu
akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
Luka 17:16
4 . Umepata / haujapata mshukuru Mungu maana bado anakufadhili .......
Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Zab 118:1
Kuna nguvu katika kumshukuru 💪💪
No comments:
Post a Comment