Sunday, August 11, 2024

NIPE MLIMA HUU (Give me that mountain)

 



Hesabu 14 :6-9

Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;
wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu.
Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali.
Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope.

JOSHUA 14:10-14

10 Sasa basi, angalia, yeye Bwana ameniweka hai, kama alivyosema, miaka hii arobaini na mitano, tangu wakati huo Bwana alipomwambia Musa neno hilo, wakati Israeli waliokuwa wakienenda barani; na sasa tazama, hivi leo nimepata miaka themanini na mitano umri wangu.
11 Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kutoka nje na kuingia ndani.
12 Basi sasa unipe mlima huu, ambao Bwana alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yumkini yeye Bwana atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, kama Bwana alivyonena.
13 Yoshua akambarikia, akampa Kalebu, huyo mwana wa Yefune, Hebroni kuwa urithi wake.
14 Kwa hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi, hata leo; kwa sababu alimwandama Bwana, Mungu wa Israeli, kwa utimilifu.

·        Caleb akiwa takriban miaka 40 alimfurahisha Mungu kwa kuwa na imani wao watachukua nchi/ardhi.......

·        Caleb  alikuwa ni miongoni kati ya spy wapelelezi 12 waliochaguliwa katika kila kabila la Israel

·        Kwakuwa alichaguliwa kuwa mmoja wa wapepelezi basi caleb  alikuwa ni mtu wa heshima katika kabila lake ndo maana alichagulia

Calebu alikuwa ni mtu jamii ya  wakenizi

Yoshua 14:6

[6]  Wakati huo wana wa Yuda walimwendea Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno BWANA alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadesh-barnea.

Mwanzo 15:18-19, 21

[18]  Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati, [19] Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni, [21] na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.

Mwanzo 36:8-11

[8]  Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu. [9] Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri. [10]  Haya ndiyo majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reueli, mwana wa Basemathi, mkewe Esau. [11] Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi.

 

 

SIFA YA KALEBU

Ø Alikuwa ni mtu jasiri Alikubali kwenda kuperereza nchi ambayo ni hatari na ngumu....

2 Timotheo 1:7

  Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Ø   Alikuwa ni mtu wa kujitoa Kufanana kwake anafananishwa na paulo

2 Timotheo 4:6-8

  Kwa maana, mimi sasa namiminwa kama tambiko, na wakati wa kuondoka kwangu umefika. [7]  Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; [8]  baada ya hayo nimewekewa taji la haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

 

 

 

Ø  Calebu alikuwa mtu wa imani na alimuamini Mungu Alisema " Mungu yupo pamoja nasi tusiwaogope "

 

Hesabu 14:9

 Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; kinga iliyokuwa juu yao imeondolewa, naye BWANA yuko pamoja nasi; msiwaogope.

Warumi 8:31

 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?

Ø Calebu alimhofu Mungu dhidi ya watu walio mzunguka

Alikubali kuwa watu wale ni hodari na niwakubwa lakini alisema Mungu yupo pamoja nasi.

 

IMANI YA CALEBU

Caleb  aliweza kumfurahisha Mungu kutokana na imani yake.

Mlima Hebron ulikuwa unamilikiwa na wanaak. Hawa walikuwa ni watu wenye size kubwa . Walikuwa ni watu wanaofahamika kuwa ni mashujaa kutokana na uhodari wao.

Calebu alimwambia joshua nipe mlima huu  nitawaondoa majitu katika mlima huu,

Kwa Calebu ule mlima ulikuwa ni changamoto hakuogopa chochote

Vitu unavyo hitaji  ili uweze kumiliki na kuupanda mlima.

1. Unaitaji kutiwa moyo/nguvu

Calebu alikubali ile kazi lakini ilikuwa ni ngumu . Ile kazi ilikuwa na uwoga mwingi na  ilikuwa unafanya ukiwa na pressure kubwa.

.Kutiwa moyo hakuondoi sura ya kuogopa bali  inakupa  kufanya kitu sahihi katika hali yako ya uwoga ,Hakuna mlima unaoweza kupata kama hutotiwa moyo.

 

Luka 22:43

Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.

Hii tunapata pale Yesu alipotaka kwenda Yerusalem alilia kwa uchungu mpaka malaika wakaja kumtia nguvu. Maana kile kikombe kilikuwa ni kikubwa .

Kuna wakati unaweza  taka kufanya kitu cha tofauti lakini ndani yako unapopata woga  unaitaji  mtu wa kukutia nguvu.

Yamkini  unataka kufungua campuni, au biashara,  usiogope yupo roho mtakatifu ambaye atakutia moyo . ... na kukutia nguvu

Kuna watu ambao wanapenda kufanya mambo  kivyao vyao .  Na hawataki kutiwa moyo na wenzao wanahisi wataonekana wazaifu. Hapana  kwenye kila hali unaitaji kutiwa moyo ..

2.  Unatakiwa uanze kufanya  jambo

Kuanza ni kupiga hatua  ya uwajibikaji  calebu ndo wa kwanza kusema  "tukawaondoshe majitu" na ni calebu aliye mpa mpango   joshua nataka kwenda kuwaondoa wana wa anak katika mlima hebron. Huwez kuyashinda majalibu kama  usipo piga hatua ya kwanza.  Watu wengi wanashindwa kusonga mbele kwa sababu hawawez kupiga hatua .Hawataki kuwa waanzilishi wa jambo.

Ni kweli kuanzisha jambo kuna gharama lakini gharama zake  hazina maumivu ukisha fanikiwa.

 Waebrania 11:8

 Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.

Ibrahimu aliambiwa na Mungu aache watu wake na kumfuata Mungu,  ni kweli ilimuuma lakini lengo la Mungu ni kumbariki Ilikuwa ngumu kwa mke wake Sarah's lakini kwasababu ibrahimu alikuwa ni different.  Alikubali......

Kutoka 3:3

Musa akasema, Nitageuka sasa niende nione kioja hiki, kwa nini kichaka hiki hakiteketei.

Moses aliona kichaka kinawaka moto akachukua hatua ya kukitazama  ndipo Bwana akaamua kuongea nae . Baada ya ile hatua Musa akawa mkombozi wa wana wa Israel. Ilikuwa ngumu kwake kwenda kuwakomboa lakini mkono Bwana ulikuwa juu yake.

 

Danieli 9:2

  katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nilifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.

Daniel alichukua hatua ya kusoma vitabu akajua miaka ya kuishi utumwani imeisha ,Mungu amekupa akili na maarifa ili uweze kufanya maamuzi  . Ukipiga hatua  ya kufanya jambo mungu atakupa  bonus .

3.  Unatakiwa kuwa na nia moja

Mithali 4 :25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.

Kwenye kila jambo ambalo ni mapenzi ya Mungu, unatakiwa ku focus na kujitoa kwa moyo na akili ili ulifanikishe,  ndicho caleb ambacho  alikifanya  , tangu akiwa na 40 yrs  mpaka 80 yrs aliwaza kupata ile ahadi aliyo pewa na musa.

4.  Unatakiwa ufanye kazi kwa  moyo wako wote

Mfalme hezekia alisema kwenye neno lake alifanya kazi kwenye nyumba ya Bwana  alifanya kwa moyo wote  

2 wafalme 20:1-6 Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza akasema,
Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.
Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana

Kalebu nae alifanya hivyo hivyo alitembea na Mungu kwa moyo wake wote

5. Unatakiwa uwe na uvumilivu

Kalebu alisubri mpaka ulipofika wakati sahihi wa Mungu , ndipo akamkumbusha Joshua  ahadi aliyopewa na mtumishi musa,

 Isaya 40 : 31  bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia

6. Usiache kukua  /kuongezeka

Mwanzo 1:28a

 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke.

Katikati ya changamoto na  mlima unaoutaka  usiache kukua na kuongezeka .  jitahidi sana kuongezeka ki fikra, elimu na ki maendeleo kwasababu wakati ukifika wa kupanda kwenye mlima unatakiwa usikose, yamkini mlima wako ni biashara, basi kabla ujafungua hiyo biashara inabidi upate maarifa mengi kuhusu biashara,

 

 

No comments:

Post a Comment

Makala nyingine

IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH

Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.  Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...