HABARI ZA YESU WA NAZARETI
The word 'grace' literally means 'favour' In Hebrew it is CHEN from a root word CHANAN - to bend or stoop in kindness to another as a superior to an inferior
Monday, November 17, 2025
HAPO SIO SEHEMU YA KUPUMZIKA
Tuesday, September 2, 2025
SAFARI YAKO BADO NDEFU
Sunday, August 11, 2024
NIPE MLIMA HUU (Give me that mountain)
Hesabu 14 :6-9
6 Na
Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao
walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;
7 wakanena
na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili
kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu.
8 Ikiwa
Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi
yenye wingi wa maziwa na asali.
9 Lakini
msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu;
uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope.
JOSHUA
14:10-14
10 Sasa
basi, angalia, yeye Bwana ameniweka hai, kama alivyosema, miaka hii arobaini na
mitano, tangu wakati huo Bwana alipomwambia Musa neno hilo, wakati Israeli
waliokuwa wakienenda barani; na sasa tazama, hivi leo nimepata miaka themanini
na mitano umri wangu.
11 Hata
sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa
aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo
sasa, kwa vita na kwa kutoka nje na kuingia ndani.
12 Basi
sasa unipe mlima huu, ambao Bwana alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe
ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa
yenye boma; yumkini yeye Bwana atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke
nje, kama Bwana alivyonena.
13 Yoshua
akambarikia, akampa Kalebu, huyo mwana wa Yefune, Hebroni kuwa urithi wake.
14 Kwa
hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi, hata leo; kwa
sababu alimwandama Bwana, Mungu wa Israeli, kwa utimilifu.
·
Caleb akiwa takriban miaka 40
alimfurahisha Mungu kwa kuwa na imani wao watachukua nchi/ardhi.......
·
Caleb
alikuwa ni miongoni kati ya spy wapelelezi 12 waliochaguliwa katika kila
kabila la Israel
·
Kwakuwa alichaguliwa kuwa mmoja wa
wapepelezi basi caleb alikuwa ni mtu wa
heshima katika kabila lake ndo maana alichagulia
Calebu
alikuwa ni mtu jamii ya wakenizi
Yoshua 14:6
[6] Wakati huo wana wa
Yuda walimwendea Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi,
akamwambia, Wewe wajua hilo neno BWANA alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu,
katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika
Kadesh-barnea.
Mwanzo 15:18-19, 21
[18] Siku ile BWANA
akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa
Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati, [19] Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni,
[21] na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.
Mwanzo 36:8-11
[8] Esau akakaa katika
mlima Seiri, Esau ndiye Edomu. [9] Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu
katika mlima Seiri. [10] Haya ndiyo
majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reueli, mwana wa
Basemathi, mkewe Esau. [11] Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na
Gatamu, na Kenazi.
SIFA
YA KALEBU
Ø Alikuwa
ni mtu jasiri Alikubali kwenda kuperereza nchi ambayo ni hatari na ngumu....
2 Timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa
roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Ø Alikuwa ni mtu wa kujitoa Kufanana kwake anafananishwa
na paulo
2 Timotheo 4:6-8
Kwa maana, mimi sasa
namiminwa kama tambiko, na wakati wa kuondoka kwangu umefika. [7] Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo
nimeumaliza, Imani nimeilinda; [8] baada
ya hayo nimewekewa taji la haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa
siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Ø Calebu alikuwa mtu wa imani na alimuamini
Mungu Alisema " Mungu yupo pamoja nasi tusiwaogope "
Hesabu 14:9
Lakini msimwasi BWANA,
wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; kinga
iliyokuwa juu yao imeondolewa, naye BWANA yuko pamoja nasi; msiwaogope.
Warumi 8:31
Basi, tuseme nini juu ya
hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?
Ø Calebu
alimhofu Mungu dhidi ya watu walio mzunguka
Alikubali kuwa watu
wale ni hodari na niwakubwa lakini alisema Mungu yupo pamoja nasi.
IMANI
YA CALEBU
Caleb aliweza kumfurahisha Mungu kutokana na imani
yake.
Mlima Hebron ulikuwa
unamilikiwa na wanaak. Hawa walikuwa ni watu wenye size kubwa . Walikuwa ni
watu wanaofahamika kuwa ni mashujaa kutokana na uhodari wao.
Calebu alimwambia
joshua nipe mlima huu nitawaondoa majitu
katika mlima huu,
Kwa Calebu ule mlima
ulikuwa ni changamoto hakuogopa chochote
Vitu
unavyo hitaji ili uweze kumiliki na
kuupanda mlima.
1.
Unaitaji kutiwa moyo/nguvu
Calebu alikubali ile
kazi lakini ilikuwa ni ngumu . Ile kazi ilikuwa na uwoga mwingi na ilikuwa unafanya ukiwa na pressure kubwa.
.Kutiwa moyo hakuondoi
sura ya kuogopa bali inakupa kufanya kitu sahihi katika hali yako ya uwoga
,Hakuna mlima unaoweza kupata kama hutotiwa moyo.
Luka 22:43
Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Hii tunapata pale Yesu
alipotaka kwenda Yerusalem alilia kwa uchungu mpaka malaika wakaja kumtia
nguvu. Maana kile kikombe kilikuwa ni kikubwa .
Kuna wakati
unaweza taka kufanya kitu cha tofauti
lakini ndani yako unapopata woga
unaitaji mtu wa kukutia nguvu.
Yamkini unataka kufungua campuni, au biashara, usiogope yupo roho mtakatifu ambaye atakutia
moyo . ... na kukutia nguvu
Kuna watu ambao
wanapenda kufanya mambo kivyao vyao
. Na hawataki kutiwa moyo na wenzao
wanahisi wataonekana wazaifu. Hapana
kwenye kila hali unaitaji kutiwa moyo ..
2. Unatakiwa
uanze kufanya jambo
Kuanza ni kupiga
hatua ya uwajibikaji calebu ndo wa kwanza kusema "tukawaondoshe majitu" na ni calebu
aliye mpa mpango joshua nataka kwenda kuwaondoa
wana wa anak katika mlima hebron. Huwez kuyashinda majalibu kama usipo piga hatua ya kwanza. Watu wengi wanashindwa kusonga mbele kwa
sababu hawawez kupiga hatua .Hawataki kuwa waanzilishi wa jambo.
Ni kweli kuanzisha
jambo kuna gharama lakini gharama zake
hazina maumivu ukisha fanikiwa.
Waebrania
11:8
Kwa
imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa
urithi; akatoka asijue aendako.
Ibrahimu aliambiwa na
Mungu aache watu wake na kumfuata Mungu,
ni kweli ilimuuma lakini lengo la Mungu ni kumbariki Ilikuwa ngumu kwa
mke wake Sarah's lakini kwasababu ibrahimu alikuwa ni different. Alikubali......
Kutoka 3:3
Musa akasema, Nitageuka sasa niende nione kioja hiki, kwa nini
kichaka hiki hakiteketei.
Moses aliona kichaka
kinawaka moto akachukua hatua ya kukitazama
ndipo Bwana akaamua kuongea nae . Baada ya ile hatua Musa akawa mkombozi
wa wana wa Israel. Ilikuwa ngumu kwake kwenda kuwakomboa lakini mkono Bwana
ulikuwa juu yake.
Danieli 9:2
katika
mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nilifahamu
hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa
Yerusalemu, yaani, miaka sabini.
Daniel alichukua hatua
ya kusoma vitabu akajua miaka ya kuishi utumwani imeisha ,Mungu amekupa akili
na maarifa ili uweze kufanya maamuzi .
Ukipiga hatua ya kufanya jambo mungu
atakupa bonus .
3. Unatakiwa kuwa na nia moja
Mithali 4 :25
Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
Kwenye kila jambo
ambalo ni mapenzi ya Mungu, unatakiwa ku focus na kujitoa kwa moyo na akili ili
ulifanikishe, ndicho caleb ambacho alikifanya
, tangu akiwa na 40 yrs mpaka 80
yrs aliwaza kupata ile ahadi aliyo pewa na musa.
4. Unatakiwa ufanye kazi kwa moyo wako wote
Mfalme hezekia alisema kwenye neno lake alifanya kazi kwenye nyumba ya Bwana alifanya kwa moyo wote
2 wafalme 20:1-6 Siku
hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa
Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza akasema,
3 Nakusihi,
Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo
mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.mambo
ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.
2 Basi
Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana
Kalebu nae alifanya
hivyo hivyo alitembea na Mungu kwa moyo wake wote
5. Unatakiwa uwe na uvumilivu
Kalebu alisubri mpaka
ulipofika wakati sahihi wa Mungu , ndipo akamkumbusha Joshua ahadi aliyopewa na mtumishi musa,
Isaya 40 : 31 bali wao wamngojeao Bwana watapata
nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka;
watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia
6. Usiache kukua /kuongezeka
Mwanzo 1:28a
Mungu
akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke.
Katikati ya changamoto
na mlima unaoutaka usiache kukua na kuongezeka . jitahidi sana kuongezeka ki fikra, elimu na ki
maendeleo kwasababu wakati ukifika wa kupanda kwenye mlima unatakiwa usikose,
yamkini mlima wako ni biashara, basi kabla ujafungua hiyo biashara inabidi
upate maarifa mengi kuhusu biashara,
Saturday, November 18, 2023
CHINI YA UONGOZI WAKE
Monday, August 14, 2023
Nyenyekevu
Luka chapter 5 verse 1 to 11
Biblia inatufundisha vitu 2
1. Unyenyekevu _petro
2. Nguvu ya Neno
Mungu hutumia watu wanyenyekevu ili kuwafanya wawe watumishi wake.
Petro aliombwa boti na Yesu ili awahubiri watu na akatoa .
Petro hakumjua Yesu ni nani, petro hakumuwazia Yesu kama ni mtumishi wa uongo. Alimpa boti kwa moyo wake wote.
Watu wengi sasa huchagua watumishi na kudharau madhehebu.... Hawana unyenyekevu wala uvumilivu, wako tayari ku comment vibaya kazi Mungu kama wao walikuwepo kipindi Mungu anampa kazi mtumishi wake.
Unyeyekevu ni njia mojawapo ambayo humfanya mtu kuwa na saburi,
Unyeyekevu ni njia mojawapo ya kujilinda dhidi ya uadui.
Tujifunze kwa petro
Tuesday, June 27, 2023
Mtume Yohana (The revelator)
Friday, December 30, 2022
KUENENDA KWA HEKIMA NDANI NA NJE YA WAAMINI
Friday, December 16, 2022
Nani aliye mlangoni mwa Moyo wako?
Friday, August 19, 2022
Friday, June 17, 2022
UTUKUFU WAKE YESU
Tuesday, May 31, 2022
Tuesday, December 28, 2021
MUUNGANIKO WA KIROHO KATI YA MAMA NA KIJANA...
Saturday, December 18, 2021
Mshukuru Mungu
Tuesday, November 16, 2021
MAOMBI YAKO YALIYOCHELEWA KUJIBIWA
Thursday, November 11, 2021
HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU
Tuesday, October 5, 2021
MUNGU YUPO NA ANAKUSIKILIZA MAOMBI YAKO.
Isaya 41:21
Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.
Mungu
anatupa nafasi sisi watoto wake tuweze kuongea kile kitu ambacho tunataka
tufanye, tufanyiwe, kitokee au kisitokee.
Hoja zenye nguvu
Mungu
anatupa ruhusa ya kujadiliana naye mambo yetu ambayo tunataka kumshilikisha.
Mungu
anataka tutumie akili na moyo pale tunapo taka kusema naye,
Tunapoenda mbele za Mungu tutumie moyo ili tuweze kuweka Imani zetu kwa yeye ili tupate itaji letu.
Imani
juu ya unacho kiomba basi utapokea.
Ebrania 10 : 38
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
Imani inakaa mioyoni [ warumi 10 : 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu ]
Isaya
1:18a
Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Kwenye biblia ya
kingereza kasema come now let us settle the matter
Settle
: to reach a decision or an agreement about something, or to end a disagreement:
Hapa
bado Mungu anatusogeza karibu, kwa njia
ya kusolve tatizo , yaani kuyajenga, kuondoa tofauti zetu.
Mungu
wetu alituumba akatupa uhuru wa kufanya jambo,
Tuko tofauti na viumbe vingine, Ametupa nafasi sisi wanadamu wa kujielezea mbele zake na hii ndio maana ya upendo (uhuru)
Mathayo
7 :7
Ombeni,
nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye
huona; naye abishaye atafunguliwa.
9 Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba
mkate, atampa jiwe?
10 Au akiomba samaki, atampa nyoka?
Bado
mungu anaonyesha ukaribu na wanadamu yakuwa chochote tutapata ila tumuombe yeye.
Kuna
vitu vitatu katika mstali huu
1. Omba
( ask)
to put a question to someone, or to request an answer from someone
2. Bisha ( knock)
to repeatedly hit something, producing a noise:
3. Tafuta
( seek )
to try to find or get something, especially something that is not a physical object:
Tunao
uwezo wa kumshawishi Mungu tukiwa na Hoja zenye nguvu.
Mathayo 11:12
Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
Kjv bible
Suffereth means with unwilling permission
Violent means using force to hurt or attack
Biblia
inasema ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka
Anaposema
ufalme wa mbinguni anamaanisha;-
1. Vitu vizuri vya mbinguni
2. Mamlaka
ya kutawala ya mbinguni
3. Uhuru
ambao uko mbinguni
4. Amani
iliyokuwa mbinguni
Kuupata
kwa nguvu anamaanisha kuufanyika kazi mpaka upate,
Kuuteka
- Anaposema
kuuteka Anamaana hatupewi, ila tunachukua bila lidhaa, yaani hatukustahili
kuwanacho ila tunakuwa nacho.
- Hukustahili kupata kitu flani ila unakipata.
“Nakuombea ifike level
ambayo kuna kazi ulitakiwa kuikosa, kwakuwa unazo nguvu za rohoro uipate kwa jina la Yesu ”.
Mifano
ya watu ambao walikuwa na hoja na nguvu ambazo zilibadili mambo yao.
Ibrahimu (Mwanzo 18:19-30
19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na
nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili
kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.
20 Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora
kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,
21 basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi
cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.
22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini
Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana.
23 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye
haki pamoja na mwovu?
24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji,
utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo?
25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na
mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
26 Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki
hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na
Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.
28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye
haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona
humo arobaini na watano.
29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana
humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.
30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda
wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.
Musa
(Kutoka 32:9-14
9 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu
hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu
10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao,
niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema,
Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya
Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa
kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa
nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu
wako.
13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi
wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu
mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi
chenu nao watairithi milele.
14 Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba
atawatenda watu wake.
Mfalme
Hezekia (Isaya 38:2-6)
2 Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake
ukutani, akamwomba Bwana,
3 akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba
nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo
mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.
4 Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema,
5 Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba
yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama,
nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.
6 Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme
wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu.
Hannah
(1 Samweli 1:14-20)
14 Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini?
Achilia mbali divai yako.
15 Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni
mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina
roho yangu mbele za Bwana.
16 Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa
kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo
nilivyonena hata sasa.
17 Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu
wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.
18 Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni
pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake
haukukunjamana tena.
19 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana,
kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana;
naye Bwana akamkumbuka.
20 Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na
kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba
kwa Bwana.
Yabesi (1 Nyakati 4:9:10)
9 Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze;
na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa
huzuni.
10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau
kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako
ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu!
Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Nakuombea yakuwa Mungu azidi kukufungulia Neema ya kuisikia sauti yake. AMEN
Saturday, March 27, 2021
Yesu kiongozi Mwema
Wednesday, March 24, 2021
MAOMBI YASIO YA UBINAFSI
Friday, November 20, 2020
UNAONA NINI JUU YA WATOTO WAKO
Tuesday, October 13, 2020
HOFU YA MUNGU
Tuesday, September 29, 2020
ROHO YA MATENGANO
Friday, May 1, 2020
MCHUNGAJI MWEMA
Monday, April 13, 2020
NEEMA ULIOPEWA SI BURE
YESU WA WATU WOTE
Thursday, March 19, 2020
YESU BADO ANATUPENDA
Saturday, December 7, 2019
BARAKA ZA KIUONGOZI
Friday, October 11, 2019
YAKUPASA UFANYE NINI UPATE KUOKOLEWA?
Pia tunasoma katika (wakorintho 5 :7) biblia iantuambia kuwa maana twaenenda kwa Imani, si kwa kuona, kwaiyo naweza sema kuwa ukombozi wa mwanadamu unaanzia ndani. Yaani utu wa ndani/ moyoni. Maana hata Mungu huangalia moyo,
(1samwel 16:7) 7 Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.
yeye haangalia kama sisi wanadamu kwa macho ya nyama, na hata Mungu akitaka kukujibu maombi yako mchakato wote uanfanywa katika utu wako wa ndani ndipo transformation inafanyika kuja kwa jinsi ya mwili. Mwanadamu ukiwa vizuri kwenye mambo ya rohoni automatical unakuwa connected na Mungu kwa sababu network ya mawasiliano yenu yanakuwa mazuri,
25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila;30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
Makala nyingine
IMPORTANCE OF OUR TESTIMONIES IN THE CHURCH
Mathayo 8:1-4 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, u...
-
amen SEMINA YA NENO LA MUNGU ILIYOFUNDISHWA NA MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE JIJINI DAR ES LAAM. SOMO: MAMBO YA KUFANYA ILI FI...
-
Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja ...
-
Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu,...

